Na Furaha John,Dodoma
CHAMA cha Mapinduzi(CCM), kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo katika kata ya Chipogolo Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma huku kikimsimamisha mgombea wake Hosea Fweda na kumnadi kwa mbwembwe.
Pia CCM imepokea wanachama wapya 800 kutoka Chama cha ACT-Wazalendo baada ya Mwenyekiti wa mkoa wa Chama hicho Weston Kaduma kubwaga manyanga na kujiunga na chama tawala.
Katika uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji, Adam Kimbisa, wanakazi wa Chipogolo wameaswa kumchagua diwani wa CCM, ili waweze kupata maendeleo kwa wakati mana kutoka kwa chama kinachoongoza serikali.
Ametoa rai hiyo Wilayani humo wakati wa uzunduzi wa kamapeni za uchaguzi mdogo wa marudio katika kata hiyo ya Chipogolo iliyoko ndani ya Jimbo la Kibakwe Wilayani Mpwapwa.
Mwenyekiti huyo, alisema, haitakuwa na maana yoyote kama watu wanaojielewa wakaamua kuchagua mgombea wa chama ambacho wakati wote madiwani wake wanapelekwa mahakamani na wabunge wake kufungwa jela.
Kimbisa amemnadi, mgombea huyo huku akisema kuwa kwanza ni kijana na pia ni msomi hivyo wananchi wa Chipogolo wanabahati ya kupata diwani msomi na wana kila sababu ya kujivunia hilo.
Amesema CCM Dodoma, ndio nyumbani kwao sasa itakuwa ajabu kama watampa ushindi na kumchagua diwani ambaye kwao ni Kilimanjaro badala ya kumchagua na kumuinua mtoto wa nyumbani ambaye amewekwa na CCM.
Pia amewataka kulinda heshima waliyopewa na rais, Dk. John Magufuli, ya kutimiza ahadi waliyoisubiri kwa muda mrefu ya kuhamishia serikali rasmi makao makuu Dodoma.
Amewasii, kuwakikisha hawafanyi makosa Novemba 26 mwaka huu, wamchague Diwani wa CCM, ili wazidi kupata maendeleo kwa wakati kutoka kwenye chama kinachoongoza serikali.
Mwenyekiti huyo, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, pia amepokea Mwenyekiti wa mkoa wa Chama ACT-Wazalendo, Weston Kaduma, ambaye amekihama chama hicho pamoja na wanachama wengine 800,kwa madai kuwa ni wababaishaji.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM- Taifa(NEC) na Mbunge wa Mtera,Livistone Lusinde, amewasii wakazi wa kata ya Chipogolo Walani Mpwapwa kutokurupuka wakati wa kuchagua Diwani katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu.
Mbunge huyo amesema hivi sasa vijana wamekuwa na mihemko na kujikuta wakikurupuka bila kutafakari na kuchagua viongozi ambao hawatakuwa na manufaa jambo ambalo linawafanya wajute kipindi chote cha utawala.
Lusinde, amesema,CCM huwa haina tabia ya kutoa lugha za matusi wakati wa kampeni kama wanavyofanya wenzao wa vyama vya upinzani hususani Chadema, bali inatekeleza kwa vitendo kwa kuibuka na ushindi wa kishindo.
Amesema, CCM inatambua kero zinazowakabili wananchi wa Chipogolo na imekuwa ikifanya jitihada ya kuzitatua wakati wote, sasa wanaokuja na kusema kuwa wanauwezo wa kumaliza kero zote mara moja ni waongo na hawana nia njema.
Kuhusu kutumia fulsa ya makao makuu amewataka kutumia fulsa ya makao makuu kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo badala ya kubweteka huku wakitegemea serikali itafanya kila kitu.
Mjumbe huyo wa NEC, amewataka kujishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo ili waweze kwenda kuuza bidhaa zao makao makuu kutokana na ongezeko la idadi ya wananchi ambao wamehamia Dodoma.
Akizungumza baada ya kukabidhi kadi hizo na kupokelewa rasmi CCM, Kaduma alisema, kama unataka amani na maendeleo utavipata CCM vyama vingine vyote ni wababaishaji.
“Baada ya kulitambua hiyo na kujiona kuwa nilikuwa nikipotea, ndio mana nimeamua kuja huku ambako najua ndiko kuna mambo yote,”alisema.
Your Ad Spot
Nov 2, 2017
Home
Unlabelled
CCM YAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA CHIPOGOLO, DODOMA
CCM YAZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA CHIPOGOLO, DODOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇