NA BASHIR NKOROMO
Mbichi na mbivu za wagombea wa uongozi ngazi za mikoa na Taifa ndani ya Jumuia ya Wazazi Tanzania, zinatarajiwa kubainika baada kikao cha Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo kitakachofanyika Oktoba 15 na 18, mwaka huu, katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
,
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah Bulembo, amewataka wote walioomba nafasi mbalimbali ngazi za mikoa hadi taifa kuhakikisha wanafika kwenye kikao hicho ili wapate fursa ya kujitambulisha na hatimaye kuchujwa kwa ajili ya kupatikana majina ya wagombea yatakayofikishwa kwenye vikao vya Juu vya Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya uteuzi zaidi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Bulembo mesema nafasi zinazowaniwa ni Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa, Makamu Mwenyekiti, Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa (Bara na Zanzibar), Wawakilishi kwenye vikao vya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za Jumuiya hiyo ngazi ya wilaya, Bulembo alisema wamepokea rufani kutoka kwenye wilaya za Kinondoni, Temeke, Arusha Mjini, Songea Vijijini, Kibaha Vijijini, Bagamoyo, Chato, Mvomero, Kahama na Mtwara Mjini.
Amesema malalamiko hayo yanawahusu wagombea walioshinda nafasi mbalimbali ngazi ya wilaya ikiwemo uenyekiti na kusisitiza kuwa ikibainika wapo wagombea waliojihusisha na vitendo vya rushwa, ushindi wao utatenguliwa.
Your Ad Spot
Oct 11, 2017
Home
Unlabelled
WAGOMBEA JUMUIA YA WAZAZI NGAZI ZA MIKOA NA TAIFA KUCHEKECHWA WIKI IJAYO
WAGOMBEA JUMUIA YA WAZAZI NGAZI ZA MIKOA NA TAIFA KUCHEKECHWA WIKI IJAYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇