LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 4, 2017

UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA AROBAINI NA TATU (43) ZA TANZANIA BARA

UCHAGUZI MDOGO WA MADIWANI KATIKA KATA
AROBAINI NA TATU (43) ZA TANZANIA BARA


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.

Mwenyekiti wa NEC  Jaji  Semistocles  Kaijage, amesema kuwa uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na Mahakama.

Jaji Kaijage amesema tume imetangaza kufanyika kwa uchaguzi huo mdogo, baada ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa kuitaarifu tume uwepo wa nafasi wazi za madiwani katika kata hizo 43 zilizoko katika halmashauri mbalimbali 36 na mikoa 19 ya Tanzania Bara.

Jaji Kaijage ameainisha  kwamba kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya. 292 kinampa mamlaka waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kuitarifu tume kuhusu kuwepo kwa uchaguzi huo mdogo wa madiwani.

Amefafanua kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Sura ya 292, Tume ya taifa ya uchaguzi ina wajibu wa kuitisha na kuendesha Uchaguzi mdogo katika Kata hizo.

“Hivyo, ninapenda kuchukua nafasi hii kutoa taarifa kuwa tume imepanga kuendesha uchaguzi mdogo katika Kata 43 tarehe 26 Novemba, 2017,” alisema Jaji Kaijage.

Amesema ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo itaanza Oktoba 26 ambapo kutafanyika uteuzi wa wagombea udiwani na kampeni za uchaguzi huo mdogo zitaanza Oktoba 27 na kumalizika Novemba 25.

Jaji Kaijage amesema Vyama vya Siasa, Wadau wote wa Uchaguzi na Wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo utakaozingatia ratiba iliyoainishwa hapo juu.

Ametoa mwito kwa vyama vya Siasa na Wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.

Kata ambazo zitashiriki kwenye uchaguzi huo ni kama ilivyoanishwa kwenye jedwali hapa chini:
Zifuatazo ni Kata 43 zitazohusika katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani:

Na

MKOA

HALMASHAURI

KATA
1.     
ARUSHA
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha
Musa
Halmashauri ya Jiji la Arusha
Muriet
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Ambureni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Ngabobo
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Maroroni
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Leguruki
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Makiba
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli
Moita
2.    2

DAR ES SALAAM
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
Mbweni
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Kijichi
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Saranga
3.     
DODOMA
Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa
Chipogolo
4.     
GEITA
Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’wale
Bukwimba
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

Senga
5.     

IRINGA
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Kitwiru
Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
Kimala
6.     

KILIMANJARO
Halmashauri ya Manispaa ya Moshi
Bomambuzi
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
Mnadani
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
Machame Magharibi
Halmashauri ya Wilaya ya Hai
Weruweru
7.     
LINDI
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi
Chikonji
Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Mnacho
8.     

MANYARA
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’
Nangwa

9.     

MBEYA
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe
Ibighi
10.  

MOROGORO
Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
Kiloka
Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Sofi
11.  
MTWARA
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Milongodi
Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara  Mikindani 
Reli
Halmashauri ya Mji wa Masasi
Chanikanguo

12.  
MWANZA
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
Kijima
Halmashauri ya Jiji la Mwanza
Mhandu
13.  
RUKWA
Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
Sumbawanga
14. 14

RUVUMA
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
Lukumbule
Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
Kalulu
Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
Muongozi
15.  
SINGIDA
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Siuyu
16.  
SIMIYU
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Nyabubinza
17.  
SONGWE
Halmashauri ya Wilaya ya Momba
Ndalambo
18.  
TABORA
Halmashauri ya Wilaya ya Nzega
Nata
Halmashauri ya Wilaya ya Urambo
Muungano
19.  


TANGA
Halmashauri ya Mji wa Korogwe
Majengo
Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto
Lukuza
Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli
Mamba


Imetolewa leo tarehe 04 Oktoba, 2017.



Jaji (R) Semistocles S. Kaijage
MWENYEKITI
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages