Waziri Tzeba akizungumza Prof. Karl-Herz Knoop |
Taasisi ya TaGEDO inayosaidia Kinamama na Vijana kuwajengea uwezo wa kujiajiri kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, imefanikiwa kuukutanisha uongozi wa kampuni ya Riela ya Ujerumani na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tzeba kwa ajili ya kuona kampuni hiyo itakavyoweza kuwekeza zaidi katika sekta ya kilimo hapa nchini.
Juzi jijini Dar es Salaam, Waziri Tzeba alikutana na mmiliki wa kampuni hiyo ya Reila Bilionea wa nchini Ujerumani Prof. Karl-Herz Knoop na msaidizi wake Klaus Kunkemoller na kufanya mazungumzo ya kina ambapo mmiliki wa kampuni hiyo ambayo tayari inalo tawi lake Himo Moshi, alieleza kuhusu azma yake kuanzisha husuasan ya kupanua teknolojia ya uhifadhi wa nafaka zinazolimwa katika maneno ya mikoa kadhaa hapa nchini yakiwemo Songea, sumbawanga.
Mazungumzo hayo pia yalihudhiriwa na baadhi ya viongozi wa TaGEDO akiwemo muasisi wa Taasisi hiyo Venance Kalumanga, Ofisa Miradi Anderson Rwela na Msemaji wa TaGEDO Petro Magoti na vijana wawili wanaofanya kazi za kujitolea hapa nchini Chath na Rosa
Knoop alimwambia Waziri Tzeba kwamba mbali na Tanzania kampuni hiyo Kampuni hiyo yenye makao makuu nchini Ujerumani imewekeza pia katika nchi za Botswana, Nigeria, Guinea, Namibia, Zambia, Sudan, Togo na Uganda,
"Tunaona fahari na furaha kubwa kupata fursa ya kuwekeza kwenye sekta ya kilimo hapa nchini Tanzania. Tanzania ni nchi ambayo ina utangamano mzuri kisiasa na sera nzuri ya uwekezaji chini ya Rais wake wa awamu ya tano Rais Dk. John Magufuli, huku ikiwa na maeneo mengi yanayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali kwa njia za kisasa", alisema Knoop.
Kwa upande wake Waziri Tzeba alionyesha kufurahishwa na namna kampuni hiyo ilivyo na teknolojia za kisasa, na ameahidi kuwa serikali itatazama namna itakavyoweza kuipa kampuni hiyo ushirikiano kuona namna itakavyoweza kutoa mchango katika kuinua uchumi wa taifa kuelekea Tanzania ya viwanda.
Kwa upande wake Muasisi wa TaGEDO ambaye ni Mhadhili katika Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kilumanga alisema amefarijika kwa uongozi wa Riela kukutana na Waziri Tzeba, akisema kwamba ikiwa kukutana huko kutazamaa matunda basi utakuwa ni sehemu ya mchango wa TaGEDO kwa taifa kwa kuwa uwekezaji utakaofanyika utaweza kutoa fursa kwa kina mama na vijana kupata ajira.
"Sisi tuliosoma tunajukumu la kuhakikisha tunaangalia kila fursa iliyosalama kuweza kuwajengea uwezo wa kujiajiri ndugu zetu hasa kinamama na Vijana ambao hawakupata fursa ya kusoma na kupata ajira, hivyo nijukumu letu kuunga mkono jitihada za Rais wetu mpendwa na mchapa kazi Dk. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha Viwanda na Uwekezaji barani Africa", alisema Kilumanga.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tzeba (kushoto) akizungumza na mmiliki wa kampuni ya Riela Bilionea wa nchini Ujerumani Prof. Karl-Herz Knoop jijini Dar es Salaam, juzi
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tzeba akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa kampuni ya Riela Bilionea wa nchini Ujerumani Prof. Karl-Herz Knoop na viongozi wa Taasisi ya TaGEDO, baada ya mazungumzo jijini Dar es Salaam, juzi
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tzeba akisisitiza jambo na mmiliki wa kampuni ya Riela Bilionea wa nchini Ujerumani Prof. Karl-Herz Knoop kabla ya kuondoka
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Charles Tzeba akiagana na mmiliki wa kampuni ya Riela Bilionea wa nchini Ujerumani Prof. Karl-Herz Knoop baada ya mazungumzo yao jijini Dar es Salaam, juzi. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇