LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 29, 2017

BURUNDI YAITAMBIA TANZANIA KATIKA SOKA MICHUANO YA UJIRANI MWEMA

 Nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Black Eagle kutoka jimbo la Makamba nchini Burundi Suleiman Mustapha (katikati) akinyanyua juu kombe la ubingwa wa mashindano ya Ujirani mwema yaliyohusisha timu nane za Tanzania na Burundi  ambayo timu hiyo ilitwaa ubingwa wengine  pichani ni Mgeni rasmi wa mashindano hayo Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Burundi Kanali Reverien Ndikuriyo (Mwenye suti nyeusi) na Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga (wa pili kushoto).
 Golikipa wa timu ya soka ya Mwamgongo kutoka Kigoma Vijijini Yaku Mussa (katikati) akitolewa nje ya uwanja na polisi baada ya kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Shomari Lawi baada ya kipa huyo kumpiga mwamuzi katika fainali ya mashindano ya ujirani mwema kati ya timu za Tanzania na Burundi ambapo Mwamgongo ilifungwa na timu ya Black eagle ya Jimbo la makamba nchini Burundi.
 Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Burundi Kanali Reverien Ndikuriyo (Mwenye suti nyeusi) akikabidhi kombe la mashindano ya ujirani mwema kwa nahodha wa timu ya Black Eagle ya jimbo la Makamba nchini Burundi Suleiman Mustapha (katikati) baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa (kushoto) Mkuu wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga
Mwenyekiti wa chama cha soka nchini Burundi Kanali Reverien Ndikuriyo (Mwenye suti nyeusi) akikabidhi kombe la mashindano ya ujirani mwema kwa nahodha wa timu ya Black Eagle ya jimbo la Makamba nchini Burundi Suleiman Mustapha (katikati) baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa (kushoto) Mkuu wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga. (Picha na Fadhili Abdallah)
--------------------------
Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TIMU ya soka ya Black Eagle kutoka jimbo la Makamba nchini Burundi imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya kwanza ya ujirani mwema unaoshirikisha timu za Tanzania na Burundi baada ya kuichapa timu ya Mwamgongo ya Kigoma Vijijini kwa bao 1-0.

Katika mchezo huo wa fainali uliofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma timu ya Mwamgongo itabidi ijilaumu kwa kushindwa kutumia vyema nafasi nyingi ilizopata ambazo kama wachezaji wake wangekuwa makini timu hiyo ingeibuka na ushindi huo.

Hata hivyo timu ya Mwamgongo itabidi ijilaumu kwa uzembe wa golikipa wake Yaku Mussa ambaye alileta Mbwembwe za kudaka mpira ulioelekezwa golini kwake hali ilifanya mpira kuangukia miguuni mwa mshambuliaji wa Black Eagle Shaka Bienvenie aliyeukwamisha mpira huo wavuni kiulaini.

Kufuatia goli hilo golikipa huyo wa Mwamgongo alimvamia na kumpiga Mwamuzi wa mchezo huo Shomari Lawi ambaye ni Mwamuzi wa ligi kuu ya Tanzania akitokea mkoa Kigoma hali iliyomlazimu mwamuzi huyo kumpa kadi nyekundu golikipa huyo wa Mwamgongo ilia toke nje ya uwanja.

Aidha baada ya kadi hiyo haikuwa kazi rahisi kumtoa golikipa Mussa kwani alipania kufanya vurugu zaidi na kumvania Mwamuzi wa mchezo huyo hali iliyolazimu polisi wa usalama waliokuwa uwanjani hao kuvamia uwanja na kumtoa uwanjani kwa nguvu golikipa huyo jambo ambalo lililaaniwa na viongozi na wapenzi wa michezo kutokana na kitendo cha utovu wa nidhamu wa golikipa huyo.

Katika mashindano hayo timu ya Black Eagle ambayo ilikuwa timu pekee iliweza kupita kwenye hatua ya robo fainali ilizawadiwa kombe la fedha taslim kiasi cha shilingi milioni 2.5 huku timu ya Mwamgongo iliyoshika nafasi ya pili ikondoka na fedha taslim milioni mbili.

Timu ya Kombaini ya Kasulu iliyoshika nafasi ya tatu ilizawadiwa pesa taslim kiasi cha shilingi 1.5 ambapo zawadi zote hizo zilitolewa na Ndiku Foundation Part inayosimamia na Mke wa Mwenyekiti huyo wa Chama cha soka nchini Burundi.

Akizungumza baada ya mashindano hayo Mwenyekiti huyo wa chama cha soka nchini Burundi,Kanali Reverien Ndikuriyo ambaye pia ni Spika wa bunge la Seneti la nchini Burundi alisema kuwa hii ni awamu ya kwanza ya mashindano hayona kwamba watakaa na viongozi wenzao wa Tanzania kuona namna ya kuboresha uendeshaji wa mashindano hayo sambamba na kuboresha zawadi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kigoma Emanuel Maganga alisema kuwa mashindano hayo yamekuwa na mafanikio makubwa katika kukuza upendo,umoja na mshikamano baina ya viongozi,wananchi na wanamichezo wa nchi zote mbili na kwamba kwa mara nyingine mashindano hayo yatapewa nafasi kwa kufanyiwa maboresho makubwa.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages