Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Agness Mtei akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ya namna vitambulisho vya Taifa vinavyotengenezwa mara baada ya kuzinduzi zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Katibu wa Cha Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Philiph Elieza akitoa salama za chama kwa wananchi kwenye mkutano wa hadhara wakati wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe akitoa salamu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Afisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi Bi Agness Mtei akisoma taarifa ya zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Maafisa wa NIDA Wilaya ya Ikungi wakiwasalimu wakazi wa kijiji na Kata ya Dung'unyiwakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika. Kulia ni Agness Mtei, Doris Niyukuri na Mary Maputa
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Ndg akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Wananchi Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wananchi mara baada ya kuwasili Kijiji na Kata ya Dung'unyi wakati wa zoezi la usajili na utambuzi kwa wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa katika Kijiji na Kata ya Dung'unyi.
Na Mathias Canal,
Singida
Zoezi
linalotekelezwa na serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
iliyo chini ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi la usajili na utambuzi wa watu
wanaoishi katika Wilaya ya Ikungi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea
limezinduliwa rasmi huku wananchi wakihamasishwa kutoa ushirikiano katika zoezi
Hilo.
Zoezi Hilo
litatekelezwa katika awamu nne ambapo katika awamu ya kwanza utekelezaji wake
utakuwa katika Tarafa ya Ikungi yenye Kata sita kwa wananchi wapatao 45,599,
Awamu ya Pili itakuwa Ni Tarafa ya Sepuka yenye Kata Saba na wananchi wakiwa Ni
49,035, Awamu ya Tatu Ni Tarafa ya Ihanja yenye Kata nne huku wananchi wakiwa
54,887 na awamu ya nne itakuwa katika Tarafa ya Mungaa yenye Kata Saba na jumla
ya wananchi wapatao 35,311.
Akizungumza Katika
Kijiji na Kata ya Dung'unyi kwenye uzinduzi wa zoezi la usajili na utambuzi kwa
wananchi kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya Taifa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Mhe Miraji Jumanne Mtaturu alisema kuwa zoezi Hilo linalenga kupata taarifa
sahihi za watu zitakazotumiwa na mifumo Yote ya serikali na binafsi
kubadilishana taarifa kwa lengo la kuboresha Huduma na kuinua hali za watu
kutoka kipato Cha chini kwenda Cha Kati.
Alisema umuhimu wa
zoezi Hilo Ni Kuimarisha ulinzi na usalama wa Nchi hususani maeneo ya mipakani,
Wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji Mali hususani
Biashara, usalama katika miamala ya kibenki pamoja na kuwezesha wananchi
kukopeshana kirahisi, Upatikanaji kirahisi wa pembejeo na zana za Kilimo, na
Wananchi katika Kaya maskini kutambulika haraka na kupata misaada kupitia
TASAF.
Umuhimu mwingine
Ni Upatikanaji wa mikopo ya elimu ya just, Kupunguza ukiritimba katika
upatikanaji wa Huduma za Jamii na Kupunguza serikali gharama za kusafirisha
daftari la wapinga kura na kuwa na daftari lenye taarifa sahihi za watu na
mahali walipo.
Mhe Mtaturu
aliwataka wananchi kutoa taarifa sahihi na kutoa ushirikiano wa karibu kwa
viongozi, Wataalamu na wasimamizi wa zoezi Hilo waliokasimishwa jukumu la
usajili.
Alisema kuwa
wananchi wote wanapaswa kuwa na viambatanisho muhimu ambavyo Ni Cheti Cha
kuzaliwa, Kadi ya kupinga kura, Vyeti vya shule, Pass ya kusafiria (Passport), Leseni
ya udereva, Kadi ya Bima ya Afya, Kadi ya Mfuko wa hifadhi ya jamii, Nambari ya
utambulisho ya mlipa Kodi na Kitambulisho Cha Mzanzibari Mkaazi.
Alisema kuwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli ameagiza
kufanyika kwa zoezi Hilo Bure kote nchini ili wananchi waweze kupata haki yao
ya Msingi ya kusajiliwa na kutambulika katika Taifa lao.
Mhe Mtaturu
alisisitiza kila mmoja kukemea kwa vitendo viashiria vyote vya Rushwa, ama
udanganyifu utakaofanywa na wachache wasioitakia mema Nchi kwa kuzorotesha
zoezi Hilo.
Katika kuhakikisha
zoezi linafanyika Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Kupitia Ofisi ya
Wilaya ya Ikungi inakamilisha jukumu lake la kusajili wananchi ambao Ni Raia
halali pamoja na uchukuaji wa alama za kibaiolojia katika awamu zote nne.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇