LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 17, 2017

BRAZIL YAISAMEHE TANZANIA DENI LA DOLA MILIONI 203 ZA MAREKANI SAWA NA SH. BILIONI 443.



1. Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi akibadilishana mkabataba na Wakili wa serikali ya Brazili Sonia Nunes, baaya kusaini   Mkataba wa msamaha wa deni la Tanzania kwa Serikali ya Brazil  wa Dola Milioni 203 za Kimarekani (sawa na Sh. Bilioni 443).

--------------

Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya Dola za Marekani milioni 203 ambazo ni sawa na shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni 445. 

Deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja Riba.

Balozi wa Tanzania Nchini Brazil Dk. Emmanuel Nchimbi alisaini mkataba huo kwaniaba ya Tanzania huku Wakili wa Hazina ya Taifa Dk. Sonia Portella Nunes akisaini kwa niaba ya Serikali ya Brazil.

Kufuatia tukio hilo, Balozi Nchimbi alishukuru Serikali ya Brazil kwa Msamaha huo ambao alisema umeunga mkono jitihada za Rais Dk. John Pombe Magufuli kujenga uchumi imara wa Tanzania.

Aliihakikishia Serikali ya Brazil utayari wa Tanzania katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi na nchi hiyo.

Kiongozi wa ujumbe wa Brazil kwenye hafla hiyo Guilheme Laux, Undersecretary of Credit and Guarantee kutoka Wizara ya Fedha ya Brazil alimtamka rasmi kufunguliwa kwa milango ya ushirikiano wa kifedha na kibiashara iliyokuwa imefungwa kutokana na deni hilo lililofanya Tanzania kuwa moja ya nchi zenye madeni sugu ya Brazil.

Hivyo kutoka sasa kampuni za Brazil zinaruhusiwa kukopa katika Benki za Brazil kwa ajili ya kutekeleza miradi nchini Tanzania lakini pia Serikali ya Tanzania inaruhusiwa kuanzisha majadiliano ya miradi mipya ya maendeleo.

 BaloziDk. Emmanuel Nchimbi akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo na Serikali ya Brazil.



1BaloziDkt. Emmanuel  Nchimbi na Mkuu wa Ujumbe wa Serikali ya Brazil Guilheme Laux (kulia kwa Balozi Nchimbi) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wapande zote mbili (Tanzania na Brazil)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages