Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Sikonge Mjini leo Agosti.10.2017 katika viwanja vya Tasaf Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi
Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya wamiliki wa maduka ya madawa ya binadamu na watumishi wa sekta ya afya wanaochukua dawa ambazo zinapaswa kupelekwa katika Hospitali za Serikali ili kuwahudumia wananchi na kuziweka katika maduka yao.
Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara na wananchi katika Kiwanja cha TASAF.
Alisema kuwa vitendo hivyo ndivyo vimekuwa vikisababisha upungufu wa dawa katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Serikali na kufanya baadhi ya wananchi kuendelea kuteseka na maradhi kwa sababu ya kushindwa gharama za ununuzi wa dawa katika maduka ya watu binafsi.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa aliwaonya watumishi wa afya na wamiliki hao wenye tabia hizo kuacha mara moja endapo watabainika kuendesha vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali.
Alisema kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili kununua dawa ili zinasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wake lakini kuna baadhi ya watumishi wa afya wasio waadirifu ambapo wamekuwa wakitorosha dawa na kuwauzia wamiliki wa maduka ya dawa na ksuababisha upungufu katika vituo vya Serikali.
Waziri Mkuu kuwa Serikali haiwezi kuwavilimia watumishi wa afya wasio waaminifu wanaochukua dawa na kuzipeleka katika maduka binafsi huku wakisababisha upungufu katika baadhi ya hospitali za umma.
Alisema kuwa hospitali ni lazima ziwe na dawa za kutosha ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameikabidhi Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora orodha ya watu wenye tabia ya kuwarubuni wakulima wa tumbaku na kununua katika mfumo ambao si rasmi na kisheria (soko huria) na kuwanyonya ili wahojiwe.
Alisema kuwa watu hao kwa muda mrefu ndio wamekuwa wakiwanyonya wakulima kununua tumbaku zao kwa vishanda na kuwa fedha ambazo zinazidi kuwakandamiza.
“Nina majina ya watu ambao wamekuwa wakipita kwa wakulima na kununua tumbakuza wakulima kwa njia ya vishada ….huku wakiwanyonya kwa kuwapa fedha kidogo nawataka waache mara moja.” Alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.
Aliongeza “leo siwataji majina yao lakini nakuachia Mkuu wa Mkoa ili wewe na Kamati yako ya Ulinzi na Usalama muwaite na kuwahoji na kisha ziwaonye wasiendelee na biashara hiyo, kama wanataka kuendelea na uuzaji wa tumbaku wahakikishe wanayopeleka sokoni ni ile waliolima wenyewe na sio ya kununua kwa wakulima”
Aidha Waziri Mkuu alitoa onyo kwa watumishi wa umma ambao wamekuwa na tabia ya kugonja wakulima walime tumbaku na wakisha kuvuna na kukausha wao wanakwenda kununua kwa ajili ya kuipeleka katika makampuni ya tumbaku.
Alisema mtumishi hakatazwi kulima kulima tumbaku bali atakiwi kununua tumbaku kutoka kwa mkulima.
Waziri Mkuu huyo aliwaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kukamata watu wote wanajihusisha na ulanguzi wa tumbaku ya wakulima na kuongeza kuwa watakamatwa wakiwa na tumbaku ya ulanguzi ichukuliwe pamoja na chombo cha usafiri kinachotumika kusafirishia.
Alisema kuwa tumbaku yote inauzwa kupitia vyama vya msingi na kila mtu atauza tumbaku kwa kiwango alicholima.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇