Shamba
la miti la Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza
utafiti wa kugema utomvu wa miti ya msindano kama njia ya kujiongezea kipato.
Akizungumza
na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya tabia ya nchi ya nchini Malawi
iliyotembelea Shamba la Miti la Sao Hill, Meneja wa Shamba hilo Salehe Beleko amesema
katika kuongeza vyanzo vya mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya
utafiti na ikibainika kwamba haitaathiri ukuaji wala ubora wa miti
wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato.
Akifafanua
Salehe Baleko amesema wanatarajia kuuza kila kilo moja ya utomvu kwas h. 750.
Beleko
amesema kwa kuwa ni utafiti wameanza kwanza na miti iliyokuwa tayari kuvunwa
wakiona hakuna madhara wataendelea kwenye miti michache yenye umri mdogo na matokeo
ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo.
Naye
mtaalamu wa kampuni ya uchina, Yhoung Zhoung amesema taasisi yake imefuata taratibu zote za
ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake
inahitaji miti millioni mbili kwa mwaka ilikupata ujazo wa utomvu wanauhitaji
Akijibu
swali la mke wa Rais wa zamani wa Malawi, Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe
wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya utomvu huo mtaalamu huyo
amesema baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo
hutumika kutengenezea dawa mbalimbali bazoka (chewing gum) pamoja na gel
Mjumbe
wa Kmaati hiyo, Rashid Pemba Msusa, amesema kwa mara ya kwanza wameshuhudia
matumizi mapya kabisa ya zao la mti teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini
kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa
wauhamishie Malawi
Mtaalamu wa Kampuni ya Art International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Mtaalamu wa Kampuni ya Art International, Zhoung Yhoung akitoa maelezo kuhusu zoezi la ugemaji wa utomvu kwa ujumla unaofanywa na kampuni yake (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇