Na Agness Moshi-
MAELEZO,
Ni
takribani
mwaka mmoja sasa tangu taarifa za kujengwa kwa Mradi wa Bomba la
Mafuta litakaloanzia Hoima Nchini Uganda mpaka Tanzania kwenye
bandari ya Tanga
kuenea kwenye vyombo vya habari ,mitandao ya kijamii na kwa wakazi wa
Mkoa wa
Tanga ambao ndio wahusika wakuu kwenye mradi huu japo unajengwa kwa
manufaa ya
mataifa haya mawili kwa ujumla.
Mradi huu ni moja kati ya miradi mikubwa
ambayo Nchi imeweza kutekeleza na utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani
Billioni 3.5 ambazo ni sawa na Tsh Trillioni 8 kwa fedha za kitanzania. Bomba
hili linategemewa kuwa na urefu wa kilometa 1,445 likiwa na uwezo wa
kusafirisha mapipa ya mafuta takribani 2,016,000 kwa siku na kutoa ajira zaidi
ya 1,000 na vibarua zaidi ya 30,000.
Taarifa
hizo zilianza kuwa rasmi, mnamo tarehe
14 marchi 2016 ambapo Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki
Bw.Javier Rielo alimhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuanza kwa ujenzi wa Mradi huo.
Nyota
njema ya Mradi huu ilianza kuonekana Aprili 24 ya mwaka jana, baada ya aliyekua
Waziri wa Nishati na Madini Prof.Sospeter Muhongo kurejea Nchini kutoka Uganda,
kuongea na waandishi wa habari kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kwa mradi huo.
Bwana
Muhongo alisema kuwa, kulikua na mjadala mkubwa wa kuchagua wapi Mradi huo
ujengwe na wapinzani wakubwa kwa Tanzania walikua Kenya lakini kutokana na ubora wa
bandari ya Tanga ukilinganisha na bandari nyingine Tanzania ilichaguliwa
kunufaika na mradi huu.
“Bandari ya Tanga ni bora kwa sababu ina kina
kirefu ambacho ni zaidi ya mita 23 ambayo ndicho kinayotakiwa Kimataifa
kwasababu hiyo kinaweza kufanya kazi mwaka mzima”, alisema Prof. Muhongo.
Chagizo
la kuanza kwa mradi huu lilipamba moto
Marchi 28 mwaka huu, baada ya Rais Magufuli kukutana na Mawaziri wa Nishati
na Madini wa Serikali zote mbili katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri Ikulu, Jijini
Dar es Salaam ili kujadili Maendeleo ya Mradi huo.
Wahenga
walisema “Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha” wakiwa na maana kila kitu kikubwa
kilianza kikiwa kidogo vivyo hivyo Mradi huu ulianza kwa ahadi, makubaliano na
hatimaye utekelezaji.
Mei 21 mwaka
huu, Rais Magufuli na Rais wa Jamhuri ya
Uganda Yoweri Kaguta Museveni walitia rasmi saini ya tamko la pamoja ili kukamilisha
majadiliano ya vipengele vya mkataba wa utekelezaji wa mradi huo.
Wakazi
wa Mkoa wa Tanga, wanahesabu miezi miwili tangu kusainiwa rasmi kwa mkataba wa mradi huo utakaowapeleka kwenye
mafanikio mbalimbali ikiwemo fursa za ajira , ukuaji wa kasi wa maendeleo , na
kuurudishia umaarufu uliopotea wa mji huo.
Ikumbukwe
Mkoa huo, ulikua maarufu miaka ya 1960 na 1970 kutokana uwepo wa viwanda mbalimbali ikiwemo vya uzalishaji katani
ambalo ni zao kuu la biashara mkoani humo .Lakini umaarufu huo ulipotea baada
ya viwanda hivyo kushindwa kuendelea kuzalisha bidhaa za kutosha kama vile
kiwanda cha saruji Tanga.
Licha
ya mji huu kupoteza umaarufu bado ni kivutio kikubwa cha Utalii kwani kuna Mapango
ya Amboni ambayo yamekua yakiupamba mji huo wenye kilomita za mraba 27,348 na Wilaya
10 ambazo ni Handeni Vijijini, Handeni Mjini, Kilindi, Korogwe Vijijini,
Korogwe Mjini, Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani na Tanga Mjini pamoja na
majimbo 11 ya uchaguzi ambayo ni Tanga Mjini, Pangani, Handeni, Korogwe Mjini,
Korogwe Vijijini, Lushoto, Bumbuli, Mlalo, Kilindi Mkinga na Muheza.
Miaka
, na miezi ilipita hatimaye, Mkoa huo umefufua umaarufu wake kupitia Kata ya Chongoleani inayopatikana katika
moja ya Wilaya mkoani humo, yenye wakazi wapatao 4,737 , kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka 2012
,ambao pia karibu nusu ya wakazi wake ni wanufaika wa huduma ya umeme tangu
mwaka 2015 kufuatia mpango wa serikali
wa usambazaji umeme vijijini.
Agosti 5 mwaka huu (kesho), Tanga inatarajia
kurudisha sifa na umaarufu uliopotea kwa zaidi ya miaka takribani 60 kufuatia shughuli za uwekwaji wa jiwe la
msingi la Mradi itakayofanywa na Rais
Magufuli na Museveni ambao utapelekea
Nchi zote mbili kwenye mapinduzi ya
kiuchumi kwa Nchi na wakazi wa Mkoa huo kupitia fursa mbalimbali hususani
kwenye upatikanaji wa Ajira, biashara, chakula ,malazi, bima na huduma za kifedha.
Kwa
Upande wake, Mkurugenzi Wa Mawasialiano
Ikulu Bw.Gerson Msigwa ametoa wito kwa Watanzania wanaoishi mbali na Mkoa huo kufuatilia
matangazo na machapisho mbalimbali yanayotolewa ili kupata taarifa kuhusiana na
shughuli hiyo na kwa upande wa wakazi wa Mkoa huo amewasihi kuhudhuria ili
waweze kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Ifike
wakati Watanzania tujivunie na tumpongeze Rais Magufuli kwa juhudi anazozifanya
ili kuinua kipato kwa Wananchi kuanzia ngazi ya chini kwa kutengeneza fursa mbalimbali za ajira,
miundo mbinu ili kurahisha shughuli za biashara na Afya kwa ujumla badala
ya kushabikia mambo yasiyo na tija kwa
maendeleo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇