Miongoni
mwa mashamba hayo yapo ya familia ya Waziri Mkuu wa zamani Mhe. Fedrick
Sumaye ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Mke wake Ester Sumaye lenye
hekari 473 yaliyopo Mvomero Mkoani Morogoro.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameyataja
Mashamba 30 ambayo yamefutwa tangu 2003 hadi 2017, yakiwemo 14 katika
awamu hii ya tano na 16 katika awamu ya nne.
Waziri
Lukuvi amesisitiza kuwa ufutaji wa Mashamba pori ambayo hayajaendelezwa
na wakati huohuo yamekuwa kero kwa wananchi walio wengi ambao wanahitaji
yataendelea kubatishwa bila kujali jina, cheo, Kabila au dini ya mtu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇