Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania Bara, Thobias Andengenye, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa na Wakuu wa Vitengo wa Jeshi hilo.
Taarifa iliyotolewa leo na jeshi hilo, imesema katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi (ACF) Bakari Mrisho, amekuwa Mkuu wa Chuo na Mafunzo, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu (SF) Kennedy Komba, ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa na nafasi yake inachukiliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) James John toka Makao Makuu.
Imesema, Kamanda wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi (ACF) Gilbert Mvungi, amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Baraza Mvano ambaye alikuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kigoma.
Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Kamishna Msaidizi (ACF) Juma Kwiyamba amehamishiwa Makao Makuu, nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi (ACF) Christom Manyologa.
Kamishna Msaidizi (ACF) Fikiri Salla amekuwa Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Mbeya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa Usalama dhidi ya Moto.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Pwani, Mrakibu Msaidizi (ASF) Goodluck Zelote amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Tanga, nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi (ASF) Happy Shirima toka Makao Makuu.
Mrakibu Msaidizi (ASF) Fatma Ngenya amekuwa Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Manyara, anachukua nafasi ya Mkaguzi Msaidizi (A/INSP) Heriel Kimaro ambaye amehamishiwa Makao Makuu.
Uhamisho huo ni Mabadiliko ya kawaida yanayotokea ndani ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Your Ad Spot
Aug 16, 2017
Home
Unlabelled
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI L:AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA
JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI L:AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇