Mkuu wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama , akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake .(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MKUU wa wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama ametoa wiki tatu kwa kwa taasisi ,makampuni mbalimbali na wananchi waliokumbatia viwanja vyenye hati zaidi ya 1,000 pasipo kuviendeleza kuhakikisha wanafanya hivyo ndani ya muda huo .
Amezitaka taasisi na watu hao kwenda kufanya mazungumzo na makubaliano na idara ya ardhi wilayani hapo katika kipindi hicho .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na agizo hilo ,Assumpter alisema kati ya viwanja 1,080 viwanja kumi vinamilikiwa na taasisi mbalimbali bila kutimiza malengo husika .
Alifafanua kati ya viwanja hivyo 735 vipo Kibaha Vijijini na 345 vipo mji wa Kibaha.
Assumpter alitaja baadhi ya taasisi na makampuni hayo kuwa ni pamoja na CRDB makao makuu,mamlaka ya mapato Tanzania (TRA),Tanesco makao makuu na National Audit (NAO).
Taasisi nyingine ni Njuweni Institute Ltd -Kibaha,The Open university (OUT) ,SF Group Companies Ltd ,Hazina Ndogo na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa na Apex Housing Development.
Assumpter alisema ,wamechoka kuchezewa akili kwa kudanganywa miaka yote huku watu wakitumia ardhi kwa maslahi binafsi huku wilaya ikikosa mapato.
Alieleza kwamba ,Kibaha imeshakiwa mji na unakua kila kukicha ni lazima uendelezwe.
Assumpter alibainisha ,wadau na taasisi mbalimbali ziunge mkono juhudi za serikali kujenga viwanda na mahotel ili kuinua maendeleo na uchumi .
"Waje wafanye makubaliano hatuwezi kuwa na mapori ambayo yanatumika hadi na uhalifu ,akaekaidi hati yake itafutwa kwa mujibu wa sheria" alisema Assumpter .
Alisema wanaacha pori maeneo hali inayosababisha kuwa maficho ya kiuhalifu..
Hata hivyo Assumper alisema NSSF ilikuwa na eneo lenye jumla ya hekta 7.5 sawa na hekari 18 mkoani B,ambalo walilichukua kwa ajili ya kujenga makazi lakini halijaendelezwa tangu mwaka 1997 lilipomilikishwa.
“Taasisi za aina hii siwezi kuzikumbatia hata kidogo ,haki lazima itendeke ,eneo hilo tumelirudisha kwa mwenyewe na tumeinyanganya NSSF
“alisema Assumpter.
“alisema Assumpter.
Assumpter aliwaomba wawekezaji kwenda kuwekeza na kujenga viwanda wilayani hapo .
Katika hatua nyingine ,aliwataka waandishi Wa habari na chama cha waandishi hao Mkoani Pwani kushirikiana nae ili kuiendeleza Kibaha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇