Mkazi wa Kibaha, Pwani, Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo lake |
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amelazimika kukesha ofisini kwake jijini Dar es Salaaam akisikiiza kero za ardhi za wananchi wapatao 189 ambao alikesha nao.
Kaika hatua hiyo Waziri ametumia kiasi cha saa 20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi.
Licha ya Waziri Lukuvi kuanza kazi hiyo saa 2 asubuhi hadi saa 9 usiku, wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuendelea kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.
Wananachi wengi wenye matatizo kuhusiana nakero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hiyo ya kipekee ya kuonana na Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye kupatiwa ufumbuzi papo hapo.
Wananchi hao wamesifu hatua hii ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi moja kwa moja.
Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni, Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.
AWaziri atafanya ziara kama hii katika Kanda nyingine baada ya kukamilisha zoezi hilo katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani
Baadhi ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi mida ya saa tisa usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akisikiliza kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini kwake.
Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani, Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro
Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dare s salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya ardhi kutoka kwa wananchi. Picha kwa Hisani ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇