Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto)
akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni
mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti
wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Na
Erasto Ching’oro WAMJW
Katibu
Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii,
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika
kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema
hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya
utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na kuzingatia
nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka
hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza
kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala
pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika
kutimiza majukumu yao.
“Niwatake
Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika
kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha
katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha,
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi
kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa
katika uendeshaji wa vyuo.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu
yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa
kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo
haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha,
Mabughai, Monduli na Mlale
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati
waliokaa)akiwa akiwa na wakufunzi wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini wakati
wa mafunzo ya udhibiti wa viashiria hatarishi mahala pa kazi yaliyofanyikakatika Ukumbi
wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo leo 31.7.2017.
Picha
na Erasto Ching’oro WAMJW
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇