Wayne Rooney (wa pili kushoto) kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu-MAELEZO
Timu
ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake
ya siku mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania
walivyoipokea timu hiyo.
Timu
ya Everton iliwasili Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza
mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Imekuwa
ni uzoefu mpya kwangu kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais
atakuwa akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu
hiyo.
Pia
katika akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa
Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu
ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Great start to the pre-season. Special
thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney akitoa shukrani
za pekee kwa washabiki wa Tanzania.
Kwa
upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja
Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa
soka nchini.
Rooney
pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan
Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza
tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye
wanafunzi wenye mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye
ulemavu wa ngozi (Albino United).
Timu
ya soka ya Everton ilifanya ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa
kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe.
Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan
Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nche ya nchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇