Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa akikata utepe
kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la upasuaji kwenye kituo cha afya cha Nkomo
kilichopo kijiji cha Mwalushu,Wilayani Itilima-Simiyu
Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Dkt. Anold Musiba akitoa maelezo kwa Rais
Mstaafu,kulia ni Balaozi wa Japan nchini Tanzania Mhe.Masaharu Yoshida. Jengo
hilo limejengwa na Ubalozi wa Japan kupitia Taasisi ya Benjamini Mkapa na
kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 270
Rais
Mstaafu akiangalia moja ya vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji .Ujenzi
wa jengo hilo kwa asilimia kubwa itawasaidia akina mama wajawazito ambapo awali
wananchi wa kijiji hicho walikua wakitembea kilometa arobaini kwenda kupata
huduma za namna hiyo
Jengo
hilo la upasuaji linavyoonekana
-
Msimamizi wa ujenzi wa jengo hilo kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa Geofrey
Nyaluke (mwenye fulana ya jano) akitoa maelezo kwa Viongozi waliofika
kushuhudia ufunguzi wa jengo hilo
Rais Mstaafu akicheza mara baada ya
ufunguzi wa jengo hilo,kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Antony Mtaka na
kulia ni Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Daudi Njalu
Wananchi
wa kijiji cha Mwalushu wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi(hayupo pichani)
wakati wa ufunguzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Nkomo
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi(hawapo pichani)ambapo
alisema katika bajeti ya mwaka 2017/2018 Wilaya ya Itilima ametengewa kiasi cha
shilingi milioni 584 kwa ajili ya ununuzi wa dawa ukilinganisha na bajeti
iliyopita ya mwaka 2016/2017 ambapo shilingi milioni 315 zilitengwa.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria
ufunguzi huo akiwepo mke wa Rais Mstaafu Mama Anna Mkapa
Rais
Mstaafu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wa awamu ya tatu akihutubia
wananchi( hawapo pichani),ambapo aliwataka Watanzania kuongeza hali ya
kujiendeleza na kujitegemea ili kutatua changamoto zinazowakabili ili kuweza
kufufua pamoja na kukuza uchumi wan chi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇