Rais Dk. John Magufuli akifurahi wakati ameshika mfuko wake wa karanga alizonunua kwa mwanadada mmoja anayefanya biashara ya kuuza kwa kutembeza mitaani karanga hizo katikati ya jiji la Mwanza. Rais amewasili leo mjini Mwanza kuanza ziara ya siku mbili.
"Hizi nadhani zinatosha", inaelekea ndivyo alivyokuwa akisema, Rais Dk John Magufuli baada kununua karanga kwa mwanadada mmoja anayefanya biashara ya kuuza kwa kutembeza mitaani karanga hizo katikati ya jiji la Mwanza. Rais amewasili leo mjini Mwanza kuanza ziara ya siku mbili
Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea, leo
Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi katikati ya jiji la Mwanza waliokusanyika kumpokea, leo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mpira pamoja na Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela katika uwanja wa Nyamagana ambapo timu ya Buhongwa United ilikuwa ikicheza na Nyamwaga FC.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Wachezaji wa
Buhongwa Fc mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Nyamagana.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono
washabiki wa mpira wa miguu wakati akitoka katika uwanja wa Nyamagana jijini
Mwanza. PICHA NA IKULU
ALIPOWASILI
Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Mwanza, leoRais Dk. John Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Dini baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza
Rais Dk. John Magufuli akiangalia ngoma za asili kutoka kikundi cha Bujora mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza.PICHA: IKULU
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇