IGP Simon Sirro mjini Singida, leo |
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amelipongeza jeshi hilo mkoani Singida kwa juhudi za kupunguza matukio ya uhalifu yakiwemo ya utekaji wa magari kwa kiwango kikumbwa.
IGP Siro ametoa pongezi hizo leo asubuhi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kweye viwanja vya kambi ya kikosi cha kuzuia fujo (FFU) mjini hapa.
Amesema matukio ya uhalifu mbalimbali mkoani Singida yamekupungua kwa kiwango kikubwa kwa sasa, ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Hatua hii inachangia uwepo wa amani na utulivu kwa wananchi wa mkoa wa Singida hivyo kutoa fursa kuweza kujiletea maendeleo yao ya mkoa na taifa kwa ujumla” amesema.
IGP Siro amesema mafanikio hayo yamechangiwa na wananchi kwa kiwanngo kikubwa kwa kutoa ushuirikiano kwa jeshi la polisi.
Akifafanua amesema wananchi wamekuwa wakitoa taarifa sahihi na kwa wakati kwa jeshi la polisi pindi wanapobaini dalili ama matukio ya kihalifu.
“Kwa sasa kwa kweli wananchi hata ninyi waandishi wa habari mnatupa ushirikiano mzuri sana. Ushirikiano huu unachangia kazi zetu kuwa nyepesi na za mafanikio makubwa. Sasa hivi kule Kibiti mkoani Pwani, wananchi wanatusaidia mno taarifa zinazohusu mauaji ya watu wasiokuwa na hatia”, amefafanua zaidi.
IGP Siro amesema kwa sasa Tanzania inaonewa wivu na nchi jirani kwa namna tulivyo dhibiti matukio ya kihalifu na kupelekea nchi kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Wakati huo huo, Mkuu huyo wa jeshi la polisi ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee kushirikiana na jeshi hilo, kufichua baadhi ya watu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ya kihalifu ili waweze kuchukulia hatua stahiki.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati wa paredi ya polisi iliyoandaliwa kwa ajili yake leo kwenye viwanja vya Kambi ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia( FFU) mjini Singida
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akikagua baadhi ya askari wa jeshi la polisi mjini Singida leo wakati wa paredi maalum ya ukaguzi iliyoandaliwa kwa ajili yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇