Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umepokea
kwa fazaa, huzuni na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mshabiki
mashuhuri wa Timu ya Dar es Salam Youngs African Ali Yanga aliyefariki
katika ajali ya gari huko Mpwapwa mkoani Dodoma.
Aidha Umoja huo umeeleza kuwa kifo cha mwanachama huyo
machachari kimeacha pengo na majonzi makubwa katika klab yake hususan
katika uwanja wa soka la Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka amemtumia
salamu za mkono wa pole na rambirambi Katibu Mkuu wa Yanga Charles
Bojiface Mkwasa na kumuelezea masikitiko ya jumuiya hiyo kufuatia kifo
hicho.
Shaka katika taarifa yake ya hiyo alisema marehemu Ally
Yanga licha ya kuwa mwanachama maarufu pia ni mwanajumuiya ya umoja wa
vijana (UVCCM) ambapo katika maisha yake mara kadhaa amekuwa akishiriki
na kushirikishwa ipasavyo hasa nyakati za
kampeni na chaguzi kuu.
Alisema akiwa mkoani Dodoma alipata taarifa kupitia
mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Ally amepoteza maisha katika ajali ya
gari na kulazimika kuandika tanzia iliyokwenda mezani kwa Katibu Mkuu
wa Yanga katika Makao Makuu ya timu hiyo yaliopo
kwenye mkutano ya mitaa ya Jangwami na Twiga jijijini Dar es Salaam.
"UVCCM imepokea kwa huzuni, majonzi na masikitiko
makubwa kifo cha mwanachama huyo mashuhuri wa Yanga ambaye pia ni mdau
na mwanachama wa UVCCM, Ally atakumbukwa kwa mapenzi yake makubwa kwa
klab yake na kuwa mkereketwa kwa Chama Cha Mapinduzi
"Alisema Shaka.
Alisema katika maisha yake Ally alipenda ucheshi ,
masikhara, utani na uzungumzaji wa masuala ya soka huku akiipenda mno
Yanga na inapofungwa hasa na watani wao Simba, aliweza hata kutokwa na
machozi pamoja na kushindwa kula chakula
Kaimu huyo Katibu Mkuu alisema UVCCM ina wanachama wengi
ambao ni mashabiki na wanachama katika timu mbalimbali nchini kama vile
Yanga, Kagera Sugar, Simba, Pan African,Small Simba, Cosmo Politan ,
Malindi, Pamba, Azam , Red Star, Mbeya City,
JKT, Magereza na nyingine kadhaa .
"UVCCM katika soka kila mmoja yuko huru kuchagua na
kushabikia timu anayoitaka na kuipenda, jumuiya yetu ina mkusanyiko wa
wanachama na mashabiki wa Timu nyingi nchini wenye itikadi tofauti za
kisiasa 'Akisisitiza Shaka
Juzi mchana Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na Ally akapoteza maisha.
Ally Yanga anakumbukwa kutokana na mikogo ilioambatana
na mbwembwe zake kila Yanga ilipokuwa ikicheza. Alipenda sana mtindo wa
kujipaka masizi meusi usoni mwake huku akiweka kitambi cha bandia.
Mungu amlaze mahali pema Ally Yanga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇