Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umemtaka
Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Rchmond Edward Lowassa kuacha
uongo kwani hana historia ya kupigania maslahi ya umma.
Aidha, imesema madai ya lowassa kwamba aliwahidi wananchi angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi video
ya matamshi yake wakati akiwa katika mkutano wa hadhara akihutubia
mkoani Geita ikionyeaha kama kweli alitoa matamshi hayo.
Hayo yalielezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka
Hamdu Shaka alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga
jijini Dar Es Salam.
alisema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au kuzungumzia
mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma kwasababu hata kujiuzulu
kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa na sakata la
ufisadi.
Shaka alibainisha kuwa hakuna ushahidi wala kumbukumbu
inayoonyesha kuwa Lowasa siku moja aliwahi kutetea maslahi ya umma
wakati akiwa serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.
"UVCCM tumemestushwa na matamshi ya Lowasa yanayodai
wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akiwa Mkoani Geita kuwa aliwahi
kutamka kama angeshinda urais angeunda Tume ya kupitia mikataba ya
madini , hakuna ushahidi huo na hawezi kuthibitisha ni
uongo mtupu "Alisema Shaka.
Shaka alisema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati
alipokuwa waziri mkuu angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais
iundwe Tume lakini alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama
anavyotaka kuwaaminisha wananchi baada ya kuona
Rais John Magufuli akiungwa mkono kitaifa na kimataifa.
Kaimu huyo Katibu mkuu alikumbushia kuwa alichosikika
akisema Lowasa ni kwamba akiwa Rais atawakaribisha wawekezaji zaidi
pamoja na marafiki zake wenye nguvu za fedha na mitaji mikubwa ili
kuiendeleza migodi na uchimbaji wa madini ambayo itamtajirisha
kila wananchi bila kuelezea mbinu za utekelezaji huo.
"Waziri pekee jasiri, mzalendo na aliyekuwa mchapakazi
kwa bidii katika serikali ni Dk Magufuli kwani hata Lowassa alipomnadi
Dk Magufuli wakati akiwania ubunge mwaka 2005 alimtaja mbele ya
wananchi kwamba ni jembe na turufu muhimu "Alisema
Shaka.
Aidha alieleza sifa peke ya Lowassa akiwa serikali ni
tabia yake ya kumshauri jambo Rais na kama litafanyika, hugeuka na
kuwaambia watu kwamba yeye ndiye akiyemshauri Rais na kama si yeye
kisingefanyika.
Shaka alisema upo ushahidi kwamba aliwahi kumshauri
suala fulani Rais mstafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kisha akawaambia
wapambe wake kwamba yeye ndiye aliyeshauri kitendo kilichomfanya
Mwalium Julius K. Nyerere amwite kilichjambo lililomfanya
mwalimu Julius Nyerere amwite Lowassa nyumbani kwake msasani na
kumkanya.
"Lowasa aliitwa mbele ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM
Sukwa Said Sukwa nyumbani kwa mwalimu Msasani akasemwa vikali sana na
mwalimu kwa kitendo hicho pia akaonywa aache kutumia magazeti kusaka
uongozi na umaarufu"Alieleza Shaka
Pia Shaka alimtaka Lowassa kuacha tabia ya kutaka
kuvika joho lisilo na hadhi yake na akumbuke tuhuma ambazo amewahi
kurushiwa na viongozi wa chadema wakipita huku wakimnadi nchi nzima
haziwezi kufutika kwa mtindo anaotaka wa kujifagilia kwa
uzushi.
Hata hivyo kaimu katibu mkuu huyo alisema si kweli kama
ujasiri, uzalendo na utashi wa kutaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi,
kupambana na ufisadi na kupitia mikataba michafu haiwezekani kufanyika
bila katiba mpya kama anavyodai Lowasa.
"Ujasiri, uzalendo na uthubutu wa kutenda mambo yoyote
magumu hakuhitaji mabadiliko ya katiba , aidha kwa kuwepo wa katiba
mbaya au nzuri kwasababu vitu hivyo havishabihiani , katiba iliopo ni
nzuri na Dk Magufuli ataleta maajabu ya kihistoria
chini ya katiba ya sasa "Alisisitiza Shaka
Alimtaka Lowasa kufuta ndoto na matumaini kwamba
itatokea siku moja akawa Rais wa nchi hii na kuacha kueneza uzushi kuwa
alikatwa jina lake kwa kumhofia angepitia mikataba ya madini.
"Jina la Lowassa liliondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo
matumizi mabaya ya madaraka, viongozi wa CHADEMA kumnanga nchi nzima
pamoja na ukiukaji wake wa taratibu, miiko na maadili huku akitumia
nguvu za fedha kutaka ateuliwe jambo ambalo CCM
imelikataa "Alisema Shaka .
Baadhi ya vyombo vya habari jana vilimnukuu Lowassa
akimpongeza Rais Dk Magufuli kwa kuunda Tume ya kupitia mikataba ya
madini huku akijigamba naye aliwaahidi wananchi wakati kampeni akiwa
mkoani Geita kwamba akishinda urais angeunda Tume jambo
ambalo pia lilifanya jina lake kukatwa ndani ya CCM.
Source Uhuru 15/06/2017
Source Uhuru 15/06/2017
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇