LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 15, 2017

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MH. PAUL MAKONDA AZINDUA MPANGO KABAMBE WA KUIMARISHA HALI YA JESHI LA POLISI MKOANI DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na watendaji mkoa na polisi katika hafla ya upelekaji wa gari 26 ya jeshi la polisi katika matengenezo mkoani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu magari yaliyoharibika kwa ajili ya kwenda katika matengenezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo katika Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es Salaam.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu magari yaliyoharibika kwa ajili ya kwenda katika matengenezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) na watatu kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni , Ally Hapi leo katika Kituo cha Polisi Osterbay jijini Dar es Salaam.
Askari wakifuatilia tukio.
Moja ya gari mbovu ya Polisi ikiwa tayari kwa kusafirishwa kwa ajili matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa pamoja na Wanajeshi wataopeleka magari kwa ajili ya matengenezo mkoani Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika leo katika kituo cha Osterbay jijini Dar es Salaam.
 Na Mwandishi Matokeo chanyA
Katika awamu ya kwanza Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amezindua mpango wa kukarabati Magari ya Polisi yanayotumika katika doria. Amepokea magari Mabovu 26 ambayo yamesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro kuundwa upya ili kuanza kufanya kazi ya Doria. Magari hayo yatakuwa na muundo unaowawezesha askari kukaa kidoria nasio kama abiria kama ilivyosasa.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, ameahidi kukabidhi polisi vifaa vya ulinzi kama silaha za kukamata kwa kupiga shoti ya umeme, kurunzi za mwanga mkali, bastola 500 na vikinga risasi.
Makonda alipokuwa ziarani nchini Marekani, amepata vifaa vya patrol kwa ajili ya Jeshi la Polisi Mkoani Dar es Salaam ambavyo ni Baiskeli 500 na Pikipiki 200.
Katika awamu ya pili atakarabati na kuunda tena magari 30 na kufanya jumla yawe 56.
Amesema Katika magari hayo mara yatakapo kamilika yatafungwa Kamera za kufuatilia magari hayo na kutuma matukio yote ya barabarani katika picha mwendo moja kwa moja makao makuu ya polisi.
Vilevile kutafungwa komputa 8 katika vituo 20 ambapo taarifa zote zinazoripotiwa zitasajiliwa kwenye computer na wahusika/watuhumiwa kuchukuliwa picha na alama mbalimbali ambazo zitahifadhiwa katika Data Center ambayo raisi ameizindua.
Makonda ameanza na vituo vya polisi 20 sasa, kutafungwa kamera ambazo zitakuwa na uwezo wa kutuma matukio mojakwa moja kwa OCD, RPC, Kamishina wa Jeshi la Polisi na kwa Mkuu wa Mkoa ambae ni Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa Mkoa.
Kupitia kamera hizi wataona mubashara matukio yote yanayoendelea katika vituo vya polisi. Mtu akiiingia au akitoka polisi ataonekana.
Hatua hizi zitaondoa usumbufu kwa raia hasa wakati ndugu wanapomtafuta ndugu yao aliyekatika vituo vya polisi. Mfano ndugu aliyepotea au aliyekamatwa na kuwekwa mahabusu, hivyo hauta hangaika kumtafuta kila kituo bila mafanikio. Mwnanchi atakapo toa taarifa kituooni atataja jina na polisi watamtafuta kwa “search” tu kwenye mtandao wa jeshi la polisi kisha ataonekana kituo alipo ripoti.
Mkuu wa mkoa ametoa wito kwa wananchi kwamba siku mfumo utakapozinduliwa ni lazima taarifa ziandikwe kwenye computer na wala zisiwekwe kwenye makaratasi ambayo yalikuwa yanaleta usumbufu kwa wananchi.
Ili Kukomesha biasha za magendo, Mkuu wa mkoa amesema kwamba kutawekwa kamera hasa Katika bandari bubu, na stendi za mabasi.
Vilevile Mkuu wa mkoa amesema tayari ameanza kusimamia ufungaji wa kamera Katika jiji lote la Dar es salaam, hasa maeneo ya taa za barabarani ambazo zitasaidia sana kudhibiti makosa ya barabarani, Hivyo kutambua mienendo ya waendesha magari.
Vilevile Kamera Zitadhibiti mambo yafuatayo:-
• Kupunguza kazi kwa askari wanaohangaika kusumbuana na waendesha magari wanaovunja sharia za barabarani.
• Zitakomesha wizi wa kukwapuliwa pochi, mabegi, vifaa vya magari, matairi ya magari, kuvunjiwa vioo. Hivyo Vijiwe vyote vinavyouza vifaa vya magari vitasajiliwa na waeleze kwamba bidhaa wanazipata wapi?
• Kwa kushirikiana na TTCL Kutakuwa na application (APP) maalumu ya kukuonyesha hali ya msongamano wa jiji la Dar es salaam Kiganjani mwako, Hivyo itawasaidia sana madereva kuchagua njia za kupita ili kuepusha msongamano wa magari Katika njia moja.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages