Mhe Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akisain Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Mhe Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa Mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Said Mwambungu alipo fika leo kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akisain kitabu cha waombolezaji alipo wasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mery Majaliwa akisain kitabu cha waombolezaji alipo wasili nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo wakati wa ibada ya kuaga mwili wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemu Marehemu Said Mwambungu.
Baadhi ya waombolezaji walio fika Msibani wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemu nMarehemu Said Mwambungu.
Jenaza lenye Mwili wa Marehemu Said Mwambungu likiwa limefunikwa na bendela ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kusoma dua mbali mbali za kumrehemuNyumbani kwake kabla ya kusafirishwa kuelekea kijijini kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .(PICHA NA FAHADI SIRAJI)
Na Mwandishi wetu. Dar Es Salam
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema
umepata mshituko na fazaa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Mwanasiasa na kiongozi jasiri aliyejituma kulitumikia Taifa lake
kwa utii, nidhamu na bidii marehemu Said Thabit
Mwambungu.
Kaimu Katibu mkuu shaka Hamdu shaka ameyaeleza hayo
nyumbani kwa Marehemu Said Mwambungu leo wakati wa ibada ya kuaga mwili
wa marehemu Said Thabit Mwambungu kabla kusafirishwa kuelekea kijijini
kwao Malinyi Morogoro kwa mazishi .
Shaka alisema Mwambungu aliyezaliwa katika kijiji cha
Malinyi Ulanga mkoani Disemaa 5 mwaka 1955 alianza kufanya kazi katika
Umoja wa Vijana wa CCM Machi Mosi mwaka 1978 na kuthibitishwa kiajira
Januari mosi mwaka 1979 akiwa katibu msaidizi
Mkuu UVCCM Makao Makuu
Akiwa mtumishi hodari, makini na mchapakazi mahiri
aliteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa Katibu wa CCM wilaya ya Kibaha
kabla hajapanda na kuwa katibu wa ccm mkoa wa Pwani.
Shaka alisema kada huyo pia katika uhai wake aliteuliwa
kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro baadae akawa mkuu wa mkoa wa Ruvuma huku
akiacha rekodi nzuri za kiutendaji katika nafasi zote alizowahi kushika
kisiasa na kiserikali.
"Tumempoteza kiongozi shupavu, muaminifu na muadilifu,
ameyatumia maisha yake kutumikia Taifa lake kwa utii nidhamu, ameanza
safari ya utumishi akitokea UVCCM ambako alipikwa kimaadili na kizalendo
"Alieleza Shaka
Aidha Kaimu Katibu Mkuu ameitaka familia marehemu,
ndugu na jamaa kuwa wenye ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha
msiba na maombolezo kwani uamuzi na mapenzi ya mwenyezi mungu hayawezi
kuepukwa na binadamu.
Pia katibu mkuu shaka ametuma salamu za rambirambi
kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John
Magufuli na kumtakia awe mwenye subira kwa kumpoteza mwanachama
shupavu, mtendaji mahiri akiwa serikalini na kada
wa CCM aliyepevuka kisiasa na kiitikadi .
"Tunatoa mkono wa rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama
chetu na tunampa pole zetu kufuatia kifo cha mwenzetu ametutoka katika
wakati tuliokuwa tulimhitaji na kumtegemea, mungu amlaze mahali pema na
kumsamehe makosa yake " alisema shaka
Marehemu Mwambungu ambaye kitaaluma ni muandishi wa
habari gwiji, atakumbukwa jinsi alivyotoa mchango katika tasnia ya
uandishi wakati akifanya kazi katika magazeti ya chama tawala Uhuru na
Mzalendo kwa miaka kadhaa . katika kuaga mwili wa
nyumbani kwake Tabata viongozi kadhaa wamehudhuria wakiwemo Rais
Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete,
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mery Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, viongozi wa CCM na jumuiya
zake, makada na wanachi mbali mbali.
Marehemu Said Thabit Mwambungu atazikwa kesho Malinji
Morogoro baada ya sala ya alasiri. Mungu ailaze mahali pema peponi roho
yake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇