Na MatukiodaimaBlog
UMOJA wa vijana
wa chama
cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa
umepongeza hatua ya Rais
Dkt John Magufuli kutengua uteuzi
wa aliyekuwa waziri wa Nishati na
Madini Prof Sospeter Muhongo baada ya
ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa
dhahabu na kataka mawaziri
zaidi watakaohusishwa na ufisadi
kutumbuliwa .
Huku mkuu wa
mkoa wa Iringa Amina Masenza akidai
kuwa mkoa wake hauzui wananchi
kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia ila hatapenda kuona
wananchi wanaunga mkono maamuzi
mbali mbali ya Rais kwa kufanya vurugu
na kuandamana barabarani .
Akizungumza na wanahabari leo ofisini kwake juu ya tamko hilo la kumpongeza Rais Dkt Magufuli kwa kuchukua maamuzi magumu kwa
maslahi ya Taifa katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa James Mgego alisema vijana mkoani
hapa wamepokea kwa mikono
miwili uamuzi huo wa Rais wa
kumuondoa waziri Prof
Muhongo na kutaka
mawaziri na viongozi wengine
wa umma kuwajibika kwa faida ya umma na
si vinginevyo.
“ Umoja wa vijana
mkoa wa Iringa unaungana na kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na mwenyekiti
wa CCM Taifa Dkt John Pombe Magufuli kwa hatua
alizozichukua za kizalendo kwa maslahi ya watanzania kwa
kutengua uteuzi wa waziri wa
Nishati na madini ….Rais amefanya jambo
zuri ambalo linapongezwa na kila mtanzania kwa faida ya
vizazi vilivyopo na vijavyo “
Alisema kuwa Rais Dkt Magufuli amechukua uamuzi sahihi wakati
sahihi kwani nchi ilikuwa
ikipoteza raslimali nyingi
kwa ajili ya kuwanufaisha wachache
kwa maslahi yao wenyewe na sio jamii ya kitanzania .
Hivyo alisema kuwa
umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa umeona ni
vema kujitokeza mbele ya vyombo
vya habari kupinga vikali vitendo vya rushwa na ufisadi ,dhuruma
na wizi
vinavyofanywa na baadhi ya
viongozi wasio wazalendo na Taifa .
Mgego alisema UVCCM
mkoa wa Iringa haitasita kuwafichua wale
wote ambao wanaikwamisha
serikali kwa kufanya vitendo vya
ufisadi ama dhuruma dhidi ya
watanzania kwa kutumia nafasi zao
za uongozi walizo pewa .
Aidha alisema kwa kuwa
ripoti ya pili ya kiuchunguzi dhidi ya mchanga huo wa madini inakuja
ni vizuri wale
wote waliohusika kwa namna moja
ama nyingine kujitafakari na kuchukua hatua ya kujiuzulu nafasi walizopewa kabla ya kutumbuliwa na Rais .
Pia katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua
fomu za kuwania nafasi mbali
mbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza mafisadi
ambao wapo kuona
CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya chama .
Katibu wa UVCCM
wilaya ya Iringa mjini Alphonce Muyinga
alisema kuwa wanazo taarifa
za wote wanaohujumu
uchaguzi wa CCM mkoani Iringa na kuwa dawa yao inachemka kwani
hawataona haya kuwashugulikia watu hao wanaotaka kukwamisha uchaguzi huo wa CCM .
Mkuu wa mkoa wa
Iringa Masenza ambae alialikwa katika zoezi hilo la utoaji wa tamko alipongeza hatua
ya vijana hao kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Dkt Magufuli na
hata kutoa tamko hilo la pongezi .
Masenza alisema kuwa
kumekuwepo na maombi kutoka kwa wananchi wa kawaida maeneo mbali mbali ya mkoa
wa Iringa kuomba kufanya maandamano
makubwa ya kumpongeza Rais Dkt Magufuli
kwa kazi nzuri anayoifanya na maamuzi mbali mbali yenye lengo la kuwakomboa
watanzania na kuwa hakuna
kiongozi anaye zuia wao kukutana kutoa pongezi zao
kwa Rais ila si kwa kuandamana
mitaani .
“ Mimi kama mkuu wa mkoa wa Iringa nawapongeza pia wananchi wangu ambao wametambua kazi
nzuri inayofanywa na Rais wetu katika
Taifa ….nawaomba sana wananchi wenye
pongezi kwa rais ruksa kuzitoa
ila utaratibu ambao wanapaswa kuutumia ni
kukutana katika vikao vya ndani kama walivyofanya
vijana wa CCM na sio kufanya
maandamano mitaani”
|
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇