Na
Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imekusanya shilingi bilioni
63,015,450,230 kwa kipindi cha Octoba 2013 mpaka Februari 2017 tangu kuanzishwa
kwa mtambo wa kuhakiki na kusimamia Huduma za Mawasiliano(TTMS) nchini.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani
wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigamboni Mhe.Dkt Faustine Engelbert leo
Bungeni.
“Mtambo
huu umesaidia Mamlaka ya Mawasiliano nchini kuongeza ufanisi katika kusimamia
Sekta ya Mawasiliano pamoja na kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko
yanayotokea katika Sekta ya Mawasiliano Duniani kote”,Aliongeza Mhe.Ngonyani
Aidha
kati ya pesa izo bilioni 56,987,368,631 zimewasilishwa hazina na shilingi
bilioni 6,028,081,599 zimewasilishwa Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) kwa
ajili ya kugharamia tafiti mbalimbali zenye manufaa kwa nchi yetu ambapo kabla ya
hapo kahukuwa na mapato hayo.
Amesema
mtambo huu umeiwezesha TCRA kuwa na uwezo wa kusimamia mawasiliano ya simu za
Kimataifa na zile za mwingiliano,pia mtambo huo umesaidia kudhibiti mawasiliano
ya Simu za ulaghai za kimataifa na kusimamia ubora wa mitandao katika kutoa
huduma bora kwa wananchi,kudhibiti namba tambulishi za vifaa vya mawasiliano
nchini pamoja na usimamiaji wa miamala ya fedha
inayopita katika mitandao ya simu hapa nchini.
“Aidha
pamoja na mafanikio hayo jitihada za kuboresha zaidi mfumo huu ili kuweza
kubaini na kujiridhisha juu ya mapato yote yatokanayo na huduma za mawasiliano na yanayokidhi mahitaji ya
Mamlaka ya Mapato Tanzania,Benki kuu ya Tanzania na TCRA zinaendelea”Aliongeza
Mhe.Ngonyani.
Aidha Serikali itaendelea
kuwajengea uwezo wataalamu wa TCRA ili waweze kuendana na kasi ya ukuaji wa
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano hususani katika eneo hili la kuchakata
taarifa mbalimbali za huduma za mawasiliano zinazopatikana kutoka kwa watoa
huduma ili kuweza na kujiridhisha juu ya mapato yote
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇