Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum wa
chama hicho Mhe. Dr. Elly Marko Macha aliyefariki tarehe 31 Machi 2017.
Akitoa taarifa ya nafasi
hiyo kuwa wazi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe.
Semistocles Kaijage amesema kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya
Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ameijulisha Tume juu ya kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge huyo.
Amesema taratibu za kujaza
nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia Ibara ya 78 (4) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kifungu cha 86A (8) cha
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇