Iringa, Tanzania
MAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi mkoa wa Iringa imemwachia kwa dhamana aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dk. Jesca Msambatavangu (41), aliyeshitakiwa kwa kesi jinai namba 65 ya mwaka 2017.
Akisoma shitaka jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Iringa Mwanasheria upande wa Jamhuri Alex Mwita alisema kuwa Msambatavangu anadaiwa kumshambulia Neema Nyongole mkazi wa Kibwabwa katika Manispaa ya Iringa Februari 17 mwaka huu katika eneo la Kibwabwa tukio ambalo ni kinyume na kifungu cha seria kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo mwaka 2002.
Alisema upalelezi wa kesi hiyo unaendelea na kutokana na shitaka hilo upande wa Jamhuri hauna pingamizi ya dhamana kwa mshitakiwa.
Dk. Msambatavangu alikana kuhusika na tuhuma hizo huku hakimu anayesikiliza kesi hiyo David Ngunyale akisema kuwa dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi na kumtaka kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili waamini ambao kila mmoja atasaini dhamana ya sh. milioni moja.
Idadi ya wadhamini waliofika mahakamani hapo waliweza kutimiza masharti hayo na hivyo kufanikiwa kutoka kwa dhamana hadi kesi hiyo itakakapo tajwa tena mahakamani hapo June 1 mwaka huu.
Dk. Msambatavangu anayetetewa na mawakili wawili Alfred Mwakingwe na Jackson Chaula alifikishwa mahakamani hapo mda wa saa 4: 8 asubuhi kwa gari la Polisi la aina ya Toyota Land Cruiser akiwa amekaa kiti cha mbele huku nyuma kukiwa na ulinzi mkali wa askari wa kikosi cha FFU na kuingizwa mahabusu ya mahakama kwa muda kabla ya kufikishwa mahakamani.
Idadi kubwa ya wananchi walifika katika mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo, wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) walioongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wa wilaya Frank Nyalusi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe, Naibu Meya wake, huku zaidi ya watu sita wakiwa na barua za dhamana na muda wote akiwa mahakamani hapo Dk. Msambatavangu alionyesha kuwa mwenye sura ya furaha .
Your Ad Spot
May 3, 2017
Home
Unlabelled
MAHAKAMA YAMPA DHAMANA JESCA MSAMBATAVANGU
MAHAKAMA YAMPA DHAMANA JESCA MSAMBATAVANGU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇