Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa
Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akizungumza na wananchi walio jitokeza
wakati alipokuwa akifunga tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji
kwa mwanamke katika viwanja vya Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam
jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa
Wilaya ya Temeke, Phares Magesa akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata
ya Sandali, Engerasia Lyimo (kilia) wakati alipowasili katika viwanja
vya Puma kata ya Sandali Dar es Salaam jana.
Sajini wa Polisi, Mrisho Athumani (wa tatu kulia) akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (kushoto) wakati alipo alipokuwa akiwasili katika viwanja vya Puma kata ya Sandali Dar es Salaam jana. kuanzia kulia ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Zuberi Kabumaye na kushoto ni Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa
Wasanii wa kikundi cha Hisia
Threater Group wakitumbuiza wakati wa kufunga tamasha la Uelimishaji wa
kupinga unyanyasaji kwa mwanamke katika viwanja vya Puma kata ya
Sandali. Dar es Salaam juzi
Koplo wa Bendi ya Polisi Kilwa
Roard, Aleni Michael (kushoto) akitumbuiza katika tamasha la
Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji kwa mwanamke katika viwanja vya
Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam jana
Msanii wa kikundi cha Hisia, Masta
Shivo , Shangar Omary akitowa burudani ya Sarakasi wakati wa tamasha la
Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji kwa mwanamke katika viwanja vya
Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam jana
Katibu wa Kikundi cha Hisia Amina
Abdallah (kushoto) akimsakili mama ambaye hakupenda jina lake kutaja
wakati wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji kwa mwanamke
katika viwanja vya Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam jana
Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo alipokuwa akitambulisha wageni wa meza kuu
Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo alipokuwa akizungumza jambo wakati wa
wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji kwa mwanamke katika viwanja vya Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam jana

Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo akipungia mkono wananchi baada ya kutambulishwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Sandali, Engerasia Lyimo-wakati
wa tamasha la Uelimishaji wa kupinga unyanyasaji kwa mwanamke katika
viwanja vya Puma kata ya Sandali. Dar es Salaam jana
Wananchi wakipitia vipeperushi wakati wa tamasha hilo
Wasanii wakikundi cha Hisia wakitowa igizo mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), NEC wa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa
Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali Wilaya ya Temeke, Anuciatha Kayombo akizungumza jambo |
Mgeni rasmi akijisajili katika kitabu cha kupinga ukatili kwa wanawake, kulia ni Katibu wa Kikundi cha Hisia Amina Abdallah
Khamisi Mussa
MJUMBE wa Halimashauri Kuu ya Taifa Wilaya ya Temeke, Phares Magesa (MNEC), amesema wanawake wamekuwa wakihofia kutoa taarifa za unyanyasaji wa kijinsia kwenye familia zao kwa kuhofia ndoa zao kuvunjika.
Magesa aliyasema jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akifunga tamasha la Tunaweza kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya mwanamke, Kata ya Sandali jijini ambapo alifafanua endapo hayo mambo yataendelea kufumbiwa macho kwenye familia akinamama wataendelea kufanyiwa ukatili huo bila kupata msaada wa kisheria.
Aliongeza kuwa unakuta ndugu wa mme, mme wote wanamfanyia ukatili mwanamke, ila yeye kwa kuhofia ndoa yake anakaa kimya bila kutoa taaria kwenye vyombo vya kisheria.
“Mtakapofanyiwa ukatili wa aina yoyote ile toeni taarifa kwenye vituo polisi, Serikali za Mitaa, Ustawi wa Jamii, Makanisani, Misikitini na Vituo vya Msaada wa Kisheria ili muweze kusaidiwa kwa kupewa elimu,”
Aliitaka jamii kutumia fursa hiyo, kwa kufanya mabadiliko kwenye mitaa na nyumba zao kwani kufanya hivyo ukatili hautokuwepo.Aliwasisitiza wanaume kuacha ukatili huo kwani kufanya hivyo ni sawa na kufanya uharifu.
Aidha amewataka wanaume kuwaheshima na kuwadhamini wake zao na kuacha mabavu ndani ya familia na pia kuwajibika kwenye familia zao.
“Wanaume tuache unyanyasaji kwa wake zetu kwani kufanya unyanyasaji huu ni uhalifu kama ulivyo uharifu mwingine, tuwaheshimu na kuwadhamini,”alisema na kuongeza
“Kuna kina baba hawawajibiki kwenye familia zao ndio maana wamama wengi wamekuwa wakijiunga kwenye vikundi mbalimbali ili waweze kujikwamua na maisha yao.Mama zangu chukueni hatua na msilee manyanyaso ya kwenye familia na tuache kutumila mila potofu kwa kutunza siri hata unapoona jirani au mtu yeyote anafanyiwa ukatili,”alisema.
Pia aliwataka wananchi kusaidia juhudi za Rais John Magufuli za kufanya kazi kwani kufanya hivyo hata ukatili wa kijinsia hautofanyika na kwa upande wake ameamua kutoa Sh 500,000 kwa ajili ya kusaidia kuenezwa kwa elimu ya kupinga ukatili dhidi ya mwanamke nchini .
Naye, Afisa Maendeleo ya Jamii, Kata ya Sandali wilayani Temeke, Anuciatha Kayombo alisema Suala la kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake si la mtu mmoja ni la wote kwa pamoja washirikiane kutoa taarifa katika vituo vya polisi.
“Wanawake na watoto wanapigwa hadi wanaumizwa lakini watu wamekuwa wagumu kutoa taarifa katika vituo vinavyohusika ili kusaidia matatizo haya kuisha kabisa kwenye jamii ,”alisema
Mkurugenzi wa Hisia Threatr, Hamis Kussa, kampeni hiyo ambayo ilianza tangu mwezi wa pili mwaka huu ililenga kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia kwa mwanamke ili aweze kujikomboa.
Alisema tamasha hilo liliandaliwa na kikundi cha Hisia Threatr ikishirikiana na Kituo cha Msaada Sheria kwa Wanawake (WLAC) kwa lengo la kutokomeza ukatili jinsia kwenye jamii.
Mwisho

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇