LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 4, 2017

MAMA SALMA KIKWETE AAPISHWA BUNGENI

Mama Salma Kikwete, mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, amekula kiapo cha uaminifu mbele ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Aprili 4, 2017. Mama Salma aliteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa Mbunge katika nafasi 10 za Rais za kuteua wabunge. Katika tukio lingine, mumewe, Dkt. Jakaya Kikwete, amemshangaza Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, baada ya kushangiliwa kwa nguvu na wabunge, pale alipomtambulisha mbele yao. "Katika vipindi vyangu vinne kama mbunge sijawahi kuona mtu akishangiliwam namna hii". Hayo yalikuwa maneno ya Spika Ndugai, ambaye baada ya kuona nderemo, vifijo na bashasha zimezidi, alitoa rukhsa kwa wabunge kuonyesha ushangiliaji wa "kujiachia" aliwaruhusu kusimama ili kuonyesha heshima kwa kiongozi huyo mstaafu ambaye alifuatana na mmoja wa watoto wake wa kiume Ally Kikwete. Pichani mama Salma akiapishwa Dodoma jana. (PICHA NA PMO/MAELEZO)
 



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Rais Mstaafu wa awamu ya  nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa  kwa mkewe mama Salma . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Mama Salma akiwasili bungeni tayari kuapishwa. (Picha na Raymond Mushumbusi wa MAELEZO)
 Mama Salma akisindikizwa na wabunge wanawake kuelekea mbeleya bunge kula kiapo
 Mama Salma akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
 Mhe. Job Ndugai akimtambulisha Rais Mstaafu Kikwete kwa wabunge
 Rais mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete, (katikati), akiwa na mwanaye wa kiume Ally Kikwete, (kushoto) na msaidizi wake, bungeni mjini Dodoma jana Aprili 4, 2017
 Dkt. Kikwete, akiongozwa na Katibu Myeka wa Spika wa Bunge, Bw. Said Yakubu, (kushoto)
Dkt. Kikwdete na mwanaye Ally, (kulia), wakiongozwa na Katibu Myeka wa Spika, Bw. Said Yakubu kuelekea ukumbini Bungeni


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.




Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.




Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika jana Bungeni Mjini Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mama Devotha Gabriel.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa awamu ya pili  saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages