Na Jumia Travel Tanzania
Kila
ifikapo Machi 8 dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake ambapo
nchi na taasisi mbalimbali huwa na shughuli kadha wa kadha katika
kusherehekea siku hii. Kwa kawaida shirika la Umoja wa Kimataifa
Duniani, UN, huwa na kauli mbiu kwa kila mwaka katika kuadhimisha siku
hii, kwa mfano mwaka huu inasema, “Wanawake Katika Ulimwengu wa
Mabadiliko ya Kazi: Kufikia usawa wa 50 - 50 ifikapo 2030.”
Tofauti na awali, sasa hivi wanawake wamekuwa na muamko mkubwa katika kuisherehekea siku hii kwani wanaitumia vilivyo kupaza sauti zao juu ya masuala yanayowahusu.
Hivyo basi, Jumia Travel inakuletea majina ya wanawake hawa 10 wa kitanzania waliojipatia umaarufu mkubwa kupitia shughuli tofauti za kijamii wanazozifanya.
Tofauti na awali, sasa hivi wanawake wamekuwa na muamko mkubwa katika kuisherehekea siku hii kwani wanaitumia vilivyo kupaza sauti zao juu ya masuala yanayowahusu.
Hivyo basi, Jumia Travel inakuletea majina ya wanawake hawa 10 wa kitanzania waliojipatia umaarufu mkubwa kupitia shughuli tofauti za kijamii wanazozifanya.
Unapozungumzia
miongoni mwa wanawake wachache waliofanikiwa kupata nyadhifa za juu
kabisa za uongozi nchini Tanzania basi huwezi kuacha kumtaja Mama Samia
Suluhu Hassan. Huyu ni Makamu wa Rais wa kwanza mwanamke kuwahi kutokea
nchini ambapo aliupata wadhifa huo kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
uliomuweka Rais John Pombe Magufuli madarakani. Tanzania kama nchi
zingine za kiafrika kwa kiasi fulani imekuwa na kasumba ya kutomwamini
mwanamke katika kushika nyadhifa za juu za kiuongozi.
Lakini kuchaguliwa kwa Mh. Samia Suluhu kumedhihirisha kuwa hakuna lisiloshindikana endapo wanawake wakiwezeshwa, kuaminiwa na kupewa fursa.
Lakini kuchaguliwa kwa Mh. Samia Suluhu kumedhihirisha kuwa hakuna lisiloshindikana endapo wanawake wakiwezeshwa, kuaminiwa na kupewa fursa.
Miongoni
mwa wanawake wanaofanya shughuli nyingi katika harakati za kuiona jamii
ya watanzania ikisonga mbele ni Maria Sarungi Tsehai. Kumchambua Maria
kwa kila shughuli anayoifanya ni vigumu kwani itachukua muda mrefu
ingawa kitaaluma yeye ni mtaalamu wa masuala ya mawasiliano. Kati ya
shughuli kadha wa kadha anazozifanya, jina la Maria Sarungi Tsehai
lilikuja kujulikana na watanzania wengi baada ya kuteuliwa kuwakilisha
kwenye Bunge la kujadili mchakato wa katiba mpya na aliyekuwa Rais wa
awamu ya nne, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete mwaka 2014.
Maria
alichaguliwa kufuatia hamasa yake ya kuibua mijadala ya kimaendeleo
nchini Tanzania kupitia mitandao ya kijamii kama vile ‘Facebook na
Twitter’ kupitia #ChangeTanzania, na kufanikiwa kuungwa mkono na wafuasi
zaidi ya 50,000.
Kwa muda
mrefu Dr. Bisimba yupo kwenye tasnia ya sheria ambapo amekuwa kipaumbele
katika kutetea maslahi na kutoa msaada kwa watanzania wanyonge
wanaonewa na kunyimwa haki zao katika masuala mbalimbali.
Ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) nafasi ambayo yupo kwa zaidi ya miongo miwili. Mama huyu msomi aliyebobea katika masuala ya sheria amekuwa na mchango mkubwa juu ya harakati za kutetea haki na usawa katika nyanja mbalimbali.
Kupitia shughuli za kituo hicho, Dr. Helen Bisimba amekuwa ni alama na nguzo muhimu ya mapambano dhidi ya unyonge na ukandamizwaji wa haki dhidi ya wananchi wa kipato cha chini.
Ni Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) nafasi ambayo yupo kwa zaidi ya miongo miwili. Mama huyu msomi aliyebobea katika masuala ya sheria amekuwa na mchango mkubwa juu ya harakati za kutetea haki na usawa katika nyanja mbalimbali.
Kupitia shughuli za kituo hicho, Dr. Helen Bisimba amekuwa ni alama na nguzo muhimu ya mapambano dhidi ya unyonge na ukandamizwaji wa haki dhidi ya wananchi wa kipato cha chini.
Watanzania
wengi walilifahamu jina la Faraja Nyalandu baada ya kuwa mshindi wa
kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka 2004. Lakini kipindi hicho
alikuwa akijulikana kama Faraja Kota kabla ya kuolewa na aliyekuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Singida Kaskazini kwa sasa,
Mh. Lazaro Nyalandu. Faraja ni mwanamke mjasiriamali katika masuala ya
kijamii ambaye amejikita zaidi katika shughuli za kielimu ili kuwajengea
uwezo watoto na vijana kuipata huduma hiyo. Kupitia dhamira hiyo
ameweza kuzindua programu mbili za kuwawezesha wanafunzi kupata masomo
kwa njia ya maswali na majibu pamoja na maelezo ya kutosha. Huduma hizi
mbili ambazo ni ‘Makini SMS na Shule Direct,’ huwawezesha wanafunzi na
walimu kuweza kusoma na kufundisha kupitia njia za simu na mtandao na
hivyo kuepuka changamoto kama vile za uhaba wa walimu, vitabu na muda wa
kujisomea.
Jokate
Mwegelo si jina geni miongoni mwa watanzania wengi na hii ilitokana na
ushiriki wake katika mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mwaka 2006 na
kuibuka nafasi ya pili. Mbali na shughuli za urembo pia anajihusisha na
muziki, ujasiriamali, uanamitindo na mavazi, uigizaji wa filamu,
utangazaji wa luninga, ushereheshaji, na shughuli za kielimu. Jina lake
ni kubwa na hamasa kwa mabinti wanaokua kutokana na mafanikio aliyonayo.
Mpaka hivi sasa amefanikiwa kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya masuala
ya urembo na mavazi inayojulikana kama ‘Kidoti.’ Mbali na hapo
anaendesha shughuli za kusaidia jamii yake kwenye nyanja ya elimu
kupitia kampeni inayokwenda kwa jina la ‘Be Kidotified.’ Mpaka sasa
amekwishajenga viwanja vya netiboli na kikapu katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana ya Jangwani.
Doris Mollel
Jina la
Dorris Mollel limeanza kusikika na kujulikana baada ya kushinda taji la
mashindano ya Miss Singida mnamo mwaka 2014. Baada ya hapo alianzisha
harakati za kuwasaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati au miezi 9
yaani njiti ambapo alianzisha taasisi yake aliyoipa jina la Doris Mollel
Foundation mwezi Februari mwaka 2015. Lengo kuu la kuanzisha taasisi
hiyo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaozaliwa
njiti. Pia ameazimia kuielemisha jamii kwani tafiti zinaonyesha kwamba
idadi ya watoto hao ni ndogo kutokana na wazazi wengi kutokuwa na
tamaduni ya kwenda kujifungulia hospitali.
Huyu ni
Afisa Mtendaji Mkuu na Muasisi wa kampuni inayojihusisha na utengenezaji
wa ‘Ice Cream’ inayokwenda kwa jina la Nelwa’s Gelato. Mercy
alishawishika kwa kiasi kikubwa kuanzisha biashara hii baada ya kuwa
masomoni London nchini Uingereza ambapo alikuwa akivutiwa na vibanda
vinavyouza ‘ice cream.’ Alikuwa anajiuliza endapo kama akirudi nchini
atafanya kitu kama hiko kwani havikuwepo. Ametimiza ndoto hiyo na kwenda
mbele zaidi kwa kuwawezesha watanzania wengine na kuwapataia mafunzo ya
namna ya kuendesha biashara hiyo. Katika biashara hiyo Mercy hutumia
viungo vya hapa nyumbani kutengenezea ‘ice cream’ zake kama vile matunda
na karanga, hivyo kutoa ajira pia kwa wakulima.
Ongezeko
la vituo vya luninga nchini Tanzania limekuja na fursa ya kuibuka kwa
wazalishaji wa vipindi lukuki vinavyohusu masuala tofauti ya kijamii.
Joyce Kiria ni miongoni mwa watangazaji wachache wanaovuma kwa kuwa na
kipindi cha luninga kinachoivutia hadhira kubwa nchini. Kipindi chake
cha ‘Wanawake Live’ kinachorushwa kwenye kituo cha luninga cha East
African Television (EATV) kimejipatia umaarufu mkubwa hususani kwa
kujikita zaidi katika kujadili na kuibua masuala mbalimbali
yanayowakabili wanawake na kuwasaidia. Kipindi chake kimekuwa ni chanzo
kizuri na msaada mkubwa kwa wanawake wanaokumbwa na changamoto
mbalimbali na hatimaye kupatiwa msaada na serikali, taasisi au viongozi
kuchukua hatua.
Inawezekana
kuwa habari ya huyu binti ndiyo iliyowagusa watanzania wengi zaidi
nchini Tanzania kwa mwaka 2016. Maisha ya Wakonta Kapunda yalibadilika
baada ya kupata ya kugongwa na gari na mwanafunzi mwenzao siku ya
mahafali ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Korogwe, Tanga
mwaka 2012. Ajali hiyo ilipelekea kupooza mwili mzima na kumlazimu
kufanya shughuli zake kwa kutumia kichwa tu.
Kilichowagusa
wengi ni ari ya kutokata tamaa kwake ambapo aliweza kushiriki shindano
la kuandika mswada wa filamu (script) lililodhaminiwa na kampuni ya
Filamu ya Maisha ya nchini Uganda. Kwa kutumia ulimi wake aliweza
kuandika na kufanikiwa kuchaguliwa kuingia hatua ya kwanza. Alijitokeza
hadharani kuomba msaada baada ya kutakiwa kwenda visiwani Zanzibar
kushiriki mafunzo ya siku 10 ambayo yalikuwa yanagharimu takribani kiasi
cha shilingi milioni 4 za kitanzania. Wakonta alikuwa anaishi na
familia yake mkoaniRukwa na haikuwa na uwezo wa kumsafirisha mpaka
Zanzibar kwenda kujumuika na wenzake. Kupitia ushujaa wake, kutoka tamaa
na kuamini kwamba ulemavu sio mwisho wa maisha, habari za Wakonta
ziliwagusa watanzania na taasisi nyingi ambapo kampeni mbalimbali
zilianzishwa kumsaidia kutimiza azma yake.
Malkia wa
muziki wa bongo flava nchini Tanzania tangu mwanzoni mwa mwaka 2000,
Lady Jay Dee, inawezekana ndiye akawa msanii pekee wa kike aliyefanya
vizuri katika tasnia hii kwa miaka yote ambayo amekuwa akifanya kazi
hiyo. Mbali na kuyumba kidogo kwenye muziki na maisha yake binafsi miaka
michache iliyopita, Lady Jay Dee au Jide aliwadhihirishia mashabiki
wake kwamba bado anao uwezo mkubwa wa kufanya muziki. Alirudi kwa
kuachia nyimbo ya ‘Ndi Ndi Ndi’ iliyomrudisha kwa kishindo kwenye chati
mbalimbali za muziki nchini na kumfanya afanye matamasha na kuzungumziwa
kila pembe ya nchi.
Kwa
hakika Lady Jay Dee ni mwanamke ambaye aliyashinda magumu yaliyomkumba
ndani ya kipindi cha muda mchache na kufanikiwa kusimama tena. Kwa
mashabiki wa muziki wa Tanzania itabakia kuwa hakuna kama yeye
utakapozungumzia wasanii wa kike kwenye muziki waliofanikiwa zaidi na
kuwashawishi wengi kuingia kwenye shughuli hiyo.
Wapo
wanawake wengi ambao wanastahili pongezi kwa shughuli wanazozifanya
katika kuwainua wanawake wenzao na jamii kwa ujumla ambao Jumia Travel
isingeweza kuwaorodhesha hapa. Lakini kwa hao waliotajwa hapo juu ni
wazi kabisa mwanamke anaweza kufanya mambo makubwa sawa na zaidi ya
mwanaume.
Na ni
matumaini yetu kwamba itafikia kipindi ambacho hakutakuwa na dhana ya
kujadili jinsia tena ya mtu katika ufanisi wa jambo fulani kama
inavyohubiri kauli mbio ya Shirika la Umoja wa Kimataifa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇