Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza Kulia Akipeana Mikono na watendaji Mara Baada ya Kuwasili kufungua
semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe,
Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga, iliyofanyika katika katika
ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwasili katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.
Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana Wa Chama cha mapinduzi Ndg:Amani Kajuna akizungumza kumkaribisha Ndg:Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.

Makatibu wakimsikiliza kwa Makakini
Akizungumzia
kuhusu mabadiliko ya katiba CCM na kanuni za jumuiya amewahimiza
watendaji hao kutopindisha na kupotosha katika eneo lolote badala yake
wafanye kazi ya kuelimisha na kusimamia utekelezaji wake.
Amesema mabadiliko ya katiba ya CCM kimsingi yameonyesha njia, mweleko na dira ya chama katika kujimarisha kisiasa.
*"Mabadiliko
Katiba ya CCM na kanuni za jumuiya hayakuzuka kama mvua za vuli
yamefanyiwa upembuzi yakinifu, tathmini za kitaalam katika taaswira ya
sayansi ya siasa, yakitekelezwa kwa kufuata misingi yake, CCM itaendelea
kupeta miaka mia mbili ijayo "Alisema*
Akizungumzia kuhusu uchaguzi Wa ndani ya chama na jumuiya alisema.
*"Lazima
mkumbuke ninyi ndio wakurugenzi wa uchaguzi wa UVCCM katika maeneo
yenu msiende kusimamia chaguzi mkiongozwa na utashi na visasi,
fuateni kanuni, taratibu ili kuzifanya chaguzi zetu kuwa huru, za haki
na za wazi, nawakumbusha wakati wote pendeni kuishi katika matamshi
na maelekezo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt Magufuli "Alisisitiza*
Aliwakumbusha
watendaji hao wa jumuiya kuwa watakuwa na jukumu kupitia vikao vyao
vya kikatiba na kikanuni kuchuja na kuwapima wagombea kwa vigezo
stahili na si kuzoazoa watu ambao hawatokani na jumuiya wala CCM.
Kuhusu
Mali za jumuiya alisema UVCCM imeamua kuandaa semina hiyo kuwajengea
uwezo watendaji katika masuala ya uchumi na biashara, namna ya kuibua
miradi mipya, kuandaa maandiko ya miradi na usimamizi ili iwe endelevu,
namna ya kutumia fursa zilizopo kuweza kuongeza kipato cha jumuiya na
kuwatoa katika ombwe la kujiona hawezi kuendesha jumuiya bila kuomba
omba.
*"Nendeni mkabuni,
mkatunze na kulinda Mali za jumuiya ili zinufaishe taasisi
hatutamvumilia mbadhirifu au mhujumu wa mali au kutumia mamlaka yake
vibaya katika kusimamia mali hizo, hata mimi ikibainika pako pahala
nimekiuka taratibu au maelekezo kwa makusudi niko tayari kuwajibika
ili kulinda heshima na nidhamu ya Mali zetu tunahitaji kuiona UVCCM
mpya si kwa maneno tena bali ni kwa vitendo"*
Kaimu
Katibu Mkuu aliwataka vijana wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa
CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli
kwani amekuwa akipigania maslahi ya umma, kujenga uchumi imara, kutetea
haki na ujenzi wa demokrasia endelevu .
picha na FAHADI SIRAJI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇