Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete ameeleza kufurahishwa kwake baada ya kuhojiwa na Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya nchini.
Mbunge huyo amezungumza hayo jijini Dar es salaam baada ya kuhojiwa na Mamlaka hiyo, ambapo alisema roho yake imesuuzika kwani jamii imeamini kwamba hahusiki kwa namna yoyote ile na biashara hiyo haramu.
"nashukuru kwa kuhojiwa huku nimepata nafasi ya kueleza ukweli juu ya jambo hili ambalo lilishaanza kuleta taharuki katika jamii, sasa umma umejua kuwa siuzi wala sihusiki na dawa za kulevya roho yangu imesuuzika "alisema Ridhiwani
Alisema vita ya dawa ya kulevya ni kubwa na inapaswa kupigwa na kila mmoja ili kuokoa kundi kubwa la vijana ambao wanaathirika kutokana na suala hilo na kwamba kuhojiwa kwake kumemfanya awe na amani.
Msikilize hapa
Msikilize hapa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇