
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing mara baada ya kuweka jiwe
la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good
Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani. Kiwanda
hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vigae laki nane kwa siku na
mwekezaji ametumia zaidi ya Dola mil.50 katika uwekezaji huo.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho cha vigae kilichopo Mkiwa
Mkuranga mkoani Pwani.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza
jambo wakati akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda
kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika
kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani
Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kiwanda hicho cha y Vigae cha Good
Will, Huang Heng Chao kutoka kwa Kiwandani hapo.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
anapata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo kuhusu matumizi ya Gesi katika Kiwanda cha Vigae cha Good Will
kutoka kwa Kiwandani hapo

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi wa Somanga mkoani Lindi wakati akiwa ziarani lkuelekea mikoa ya
Kusini(Lindi na Mtwara).

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF
katika eneo la Somanga wakati alipokuwa akielekea Nangulukulu katika
ziara yake ya mikoa ya Kusini.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia
msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni
mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye
shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha
(CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni
moja pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye mara
baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian
na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya
kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇