
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko
Dangote mara baada ya kuwasili kiwandani hapo kwa ajili ya kuzindua
magari 580 ya kusafirisha saruji nchini.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara
baada ya kumkabidhi barua ya malalamiko kutoka kwa madereva
wanaolalamikia utoaji wa ajira hizo kiwandani hapo.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
katika viwanja hivyo vya kiwanda cha Dangote kabla kuzindua magari 580
ya kiwanda hicho yatakayosafirisha saruji nchini.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote wakikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari makubwa ya kusafirishia Saruji
kiwanda hapo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego March 5,
2017

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote mara
baada ya kukagua kiwanda chake cha Saruji mkoani Mtwara.

Mmiliki
wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote akimuonesha Rais
Dkt. Magufuli sehemu ya Kiwanda hicho pamoja na vifaa vyake mkoani
Mtwara.

Rais Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki huyo wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote.

Rais
Dkt. Magufuli akizungumza jambo na mmiliki huyo wa Kiwanda akiwa na
mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote Alhaji Aliko Dangote
wakipeperusha bendera kuashiria uzinduzi rasmi wa Magari hayo 580.

Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha
kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo March 5, 2017

Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua kituo cha
kupooza umeme kwa ajili ya kuusambaza katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego na Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇