LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Mar 17, 2017

MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA NCHI TANZANIA WAFANYA MKUTANO NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI HAPA NCHINI

Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akifungua mafunzo kwa wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaaam.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Nchini Tanzania Michael Dunford akizungumza  jambo kwenye mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliowakutanisha ili kujadili njia nzuri za kufanya kazi kwa pamoja ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya akizungumza jinsi wanavyoshirikiana na serikali ya Tanzania pindi wanapoingia wakimbizi kutoka nchi mbalimbali zinazoizunguka nchini ya Tanznaia hasa zile nchi zenye migogogro ya kisiasa.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNAIDS Dk.Warren Namara akizungumza jambo pamoja natoa data kuhusu maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini pamoja na duniani na jinsi kiwango hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya taifa.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena akiwasilisha mada  kuhusu mazingira wanayofanyia kazi pamoja na kutolea ufafanuzi kuhusu jukwa la wahariri Tanzania linavofanya kazi hasa kwenye habari za jamii kwenye mkutano wao pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa uliofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viongozi mbalimbali wa Mashirika ya umoja wa mataifa nchini Tanzania wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa nchini Tanzania wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha na wahariri mbalimbali wa habari kujadili namna ya kufanya kzi ili kufikisha ujumbe kwenye jamii.
Baadhi ya wahariri wakiwa kwenye mkutano huo
Mwakilishi wa Shirika la umoja wa mataifa la wafanyakazi Duniani (ILO) kwa nchi za Afrika Mashariki, Mary Kawar akizungumza jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Baadhi ua Wahariri wa vyombo vya habari wakiuliza maswali wa wawakilishi wa mashirika ya umoja wa mataifa nchini Tanzania
Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez akijibu maswali yaliyoulizwa na wahariri kwenye mkutano
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia. Wakimbizi (UNHCR), Chansa Kapaya akijibu maswali yaliyoulizwa na wahariri.
Mwakilishi wa Shirika la UN Women Tanzania Bi. Maria Karandenizli akitolea ufafanuzi swali lililoulizwa na mmoja wa wahariri wakuu kwenye mkutano uliowakutanisha kujadili namna ya kufanya kazi pamoja na kuwaongezea uwezo wahariri kwenye utendaji kazi wao wa kila siku.
Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu, akitolea ufafanuzi baadi ya mambo kwenye mkutano uliowakutanisha wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ulioandaliwa na mashirika ya umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakichangia mada kwenye mkutano huo
Msaidizi wa Mwakilishi wa Shirika la Idadi ya Watu UNFPA, Christine Mwanukuzi akizungumza jambo wakati wa kufunga mafunzo kwa wahariri wa habari yaliyoandaliwa na mashirika ya Umoja wa mataifa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja kati ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania pamoja na baadhi ya wahariri waliofika kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja kati ya wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania pamoja na wafanyakazi wa mashirika hayo
Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania yamewakutanisha wahariri ambao ni wanachama wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ili kujadili namna ya kufanya kazi pamoja na mashirika hayo. Mashirika ya umoja wa mataifa yaliyoshiriki kwenye mkutano huo ni UNDP, ILO, FAO, WFP, UNHCR, UN Women, nk.

Akizungumza na wahariri Mwakilishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema umoja wa mataifa uko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kuonesha mchango wao kwenye jamii. Hivyo mchango wa waandishi wa habari ni wa msingi kwao na ili kuweza kutekeleza malengo waliyojiwekea hasa kuinua uchumi wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages