Dk.
Magufuli hajatia hofu watu isipokuwa
amevuruga
uzushi na uongo wa wapinzani
Ø Ni udanganyifu
pia kudai kuwa eti haiamini CCM
Na Charles Charles
KATIKA mahojiano yake na gazeti moja
litolewalo kila siku nchini yaliyochapishwa hivi karibuni, Mwenyekiti wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Kanda wa Nyasa, Peter Msigwa alisema
kwamba Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais Dk. John Magufuli
imewafanya watu kuwa na hofu wakati wote.
Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Iringa
Mjini alisema katika upande mwingine, Rais Magufuli akiwa ni Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) nacho hakiamini ingawa ndiye kiongozi wake mkuu!
“Mwalimu (Julius Kambarage) Nyerere (aliyekuwa
Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza) hakujenga majengo, lakini fikra zake
zinadumu mioyoni mwa watu”, alisema kiongozi huyo wa Chadema ambapo, kanda
anayoiongoza inaundwa na mikoa minne ya Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma.
Alisema kutokana na kutoiamini kwake
CCM, Rais Magufuli amefanya mabadiliko ya Katiba ili kupunguza idadi ya wajumbe
wa vikao vya juu na kuongeza: “Anafanya vitu vinavyotofautiana na Chama Cha
Mapinduzi”.
Labda nianze kwa kukiri kuwa namfahamu
vizuri Peter Msigwa kama Mbunge wa Iringa Mjini, na pia akiwa Mwenyekiti wa
Chadema wa Wilaya hiyo kipindi kile maana niliishi katika jimbo hilo kwa miezi
10 mwaka 2011 nilipohamishiwa huko kikazi.
Naujua udhaifu wake kama mwakilishi wa
wananchi bungeni, mahusiano yake na wapiga kura wa jimbo hilo na chuki zake kwa
CCM, serikali yake na viongozi wake na hata yeye mwenyewe katika upande wa pili
ananifahamu vizuri mpaka kunichukia.
Naujua uwezo wake mkubwa wa kutengeneza
uzushi ama uongo wowote wa kisiasa anapodhani unaweza kukisaidia chama chake au
hata mwenyewe, halafu yupo radhi na tayari kufanya hivyo wakati wowote, mahali
popote au kwa namna yoyote ile dhidi ya CCM, serikali na hata viongozi wake
anapokuwa akiamini kufanya hivyo kutaudhalilisha upande huo ambao kwake na
Chadema yake ni kama adui namba moja na hatari zaidi.
Wakati aliyekuwa Rais wa Serikali ya
Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete alipowasili Iringa mwezi Mei, 2011, Msigwa
alipokwenda katika vikao vya bunge la bajeti ya mwaka 2011/2012 alipeleka uongo
uliowaacha wananchi wa jimbo hilo wakipigwa bumbuwazi na kile alichozungumza
kwa nguvu zake zote kinywani mwake!
Katika uongo huo, mbunge huyo alidai
siku ambayo Kiwete aliwasili Iringa, barabara inayotokea Uwanja wa Ndege wa Nduli
kwenda katikati ya mji huo ilifungwa kutwa nzima kutoka saa tano asubuhi hadi
saa 11 jioni ili kusubiri kiongozi huyo kwanza apite.
Msigwa aliyekuwa akiongea bila aibu
usoni wala haya kinywani, alisema hatua hiyo aliathiri biashara pamoja shughuli
nyingi zinazofanywa na wananchi wa jimbo hilo na sehemu nyingine.
Lakini katika ukweli halisi, Kikwete
ambaye aliwasili majira ya saa 12 za jioni na kulala kwa siku moja katika Ikulu
Ndogo mjini hapo akiwa njiani kwenda Njombe, kuhudhuria mazishi ya marehemu
mama yake mzazi na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Anne Makinda alitumiwa kutengenezea uongo wa asilimia 100 na mtu huyo.
Nasema hivyo kwa sababu nilikuwepo katika
mji huo kabla, wakati akiwasili na baada ya kuondoka kwake kwenda Njombe, na
pia nilikuwepo aliporudi tena na alipopanda ndege kutoka Iringa kuelekea Dodoma
kesho yake, saa 11.30 jioni.
Hakuna barabara iliyofungwa na polisi
eti kutwa nzima ili kupisha msafara wa Kikwete upite. Kilichofanyika ni itifaki
ya kawaida sehemu zote duniani ya kuipisha misafara yote ya viongozi wakuu wa
kitaifa wanapopita, hivyo hata siku hiyo jambo hilo halikufanyika kabla na
baada ya kupita kwake.
Kilichofanywa na polisi ni kusimamisha
magari yote barabarani wakati msafara wake ulipoanza kutoka katika uwanja huo
wa ndege kuelekea mjini, halafu njia zote ambazo zilifungwa kwa ajili hiyo
hakuna iliyochukua angalau zaidi ya dakika tano tu.
Baada ya kurejea kwake jimboni na kukuta
wananchi wamekereka, Msigwa alipokwenda katika vikao vingine vya bunge
alitengeneza uzushi mpya na safari hii dhidi ya kiongozi mmoja mwandamizi wa
CCM kwa kumhusisha na biashara haramu ya nyara za serikali.
Alifanya hivyo huku akijua na kuamini
kwamba anadanganya kwa asilimia 100, lakini kwa sababu ndio mfumo wake mwenyewe
wa kisiasa na staili ya chama chake kutafuta wanachama, wafuasi na mashabiki
bila kujali uharamu wake, Msigwa alisema hayo kwa nguvu zake zote mdomoni
ingawaje alishindwa kuthibitisha popote hadi leo kwa sababu ulikuwa ni uzushi
uliovuka mipaka.
Ndiyo maana hivi leo tena amekuja na
uzushi, uongo na upotoshaji mwingine dhidi ya CCM, serikali na Rais Dk. John
Magufuli kwa vile kufanya hivyo kwake ni kama jadi yake ya siku zote katika
maisha yake ya kisiasa.
Hata anapoitwa mchungaji, neno ambalo
lina maana ya kiongozi wa kanisa kuna wakati huwa ninajiuliza sana kiasi kwamba
naona waumini wake wana mioyo iliyojaliwa ujasiri. Nawaona ni watu wanaostahili
kupewa tuzo ya kuheshimu uvumilivu wao wa juu kabisa kwa sababu ya kukubali
kusimamiwa kiroho na kiongozi wa aina ya Msigwa.
Leo anapokuja na uzushi eti kwamba
Serikali ya Serikali ya Awamu ya Tano ambayo inaongozwa na Rais John Magufuli
imewatia watu hofu ni kauli ambayo, kwa namna zote inaweza tu kutolewa na
kiongozi wa kisiasa asiyeona aibu kusema uzushi wowote.
Ni Mtanzania gani aliyetiwa hofu na serikali
hiyo ya sasa na kutokana na nini? Wapi alikokwenda na kuambiwa na wananchi
kwamba wanaishi kwa wasiwasi?
Nafahamu kuwa kauli yake hiyo inatokana
na uzoefu wa uongozi alioupata katika chama chake, kwamba ili uonekane kiongozi
mzuri ni lazima uwe na sifa zenye ukakasi.
Mtu anayetaka kuwa kiongozi
anayekubalika ndani ya Chadema lazima awe mzushi sana, muongo sana, mpotoshaji
sana, mchonganishi sana, mchochezi sana na ambaye wakati wote na mahali popote
awe radhi na tayari kusema chochote au lolote hata kama anaamini kwamba anaweza
kusababisha umwagaji wa damu.
Hizo ndizo sifa anazopaswa awe nazo pia
Msigwa akiwa ni kiongozi mwandamizi wa Chadema ambako ni Mwenyekiti wa Kanda ya
Nyasa inayojumuisha mikoa minne ya Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma; halafu ni mbunge
na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama chake hicho.
Bila shaka analazimika kuwa na sifa hizo
kwa sababu anapaswa kutekeleza matakwa ya kisiasa ya Mwenyekiti wa Taifa wa
Chama hicho, Freeman Mbowe ambaye tangu achukue wadhifa huo mwaka 2004
ameigeuza Chadema kutoka chama makini cha siasa hadi cha kiharakati zaidi
katika shughuli zake zote.
Sina hakika sana na madai kwamba wafuasi
wengi wa Chadema wakiwemo walioshiriki kufanya vurugu za Januari 21, 2011 kule
Arusha hununuliwa ama kunyweshwa pombe ya aina ya viroba ili wapate kile
kinachoitwa “stim”, na kwamba wakishakunywa ndipo sasa wanaingia barabarani ama
kuandamana kwa kauli za ama zao ama za wale waliotumwa kwenda kuwafanyia fujo kwa
jinsi wanavyoweza.
Hao ndio inawezekana hata Msigwa naye alilenga
kuwadanganya kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imewafanya watu kuwa na hofu kwa
sababu, washirika wa kundi hilo hawana utamaduni wowote wa kujiuliza, kuhoji
wala kuomba ufafanuzi wa jambo lolote linalopandikizwa kwa nia mbaya akilini au
vichwani mwao.
Wao siku zote wanafanya au kutekeleza
chochote wanachotumwa wafanye, hivyo hata wakiambiwa kwa mfano kwamba
wakaharibu mali zao wenyewe kama nyumba zao, mashamba yao na hata vinginevyo
ili isingiziwe serikali wataitikia “people’s power”, kisha wataingia barabarani
na kufanya lolote lile kwa sababu wana hamasa ya viroba vya pombe ila bahati
mbaya sana hatimaye vimepigwa marufuku.
Kuhusu mfano wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwamba “hakujenga majengo, lakini fikra zake zinadumu
mioyoni mwa watu” kinyume na utawala wa sasa kwa hakika huo ni uelewa mdogo.
Katika uongozi wake wa miaka 23 akiwa
Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, mwasisi huyo wa taifa hakuwahi kuongoza
nchi kinyume cha sheria na Ilani ya CCM au TANU iliyoishia mwaka 1977.
Alikuwa akiongoza serikali inayotekeleza
Ilani ya Uchaguzi ya TANU na kisha Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Alikuwa akiongoza
serikali inayotokana na chama cha TANU, CCM na sera za vyama hivyo vyenyewe.
Hakuwahi hata siku moja kuongoza
serikali iliyotokana na chama kingine chochote cha siasa isipokuwa hivyo
viwili, kila kimoja kwa muda wake na hivyo hawezi akaangaliwa, kupimwa wala kufanyiwa
tathmini ya uongozi kwa kutumia jina lake au sura yake binafsi isipokuwa Sera
na Ilani za Uchaguzi za TANU na CCM.
Katika hali hiyo, Msigwa anapokuja na
kauli inayohusu uongozi mahiri au makini wa Baba wa Taifa ajue kuwa anaongelea
Sera, Ilani za Uchaguzi na serikali za TANU ama CCM na siyo vinginevyo.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa pia kwa Serikali
ya Awamu ya Pili, Serikali ya Awamu ya Tatu na Serikali ya Awamu ya Nne. Zote
zilikuwepo madarakani na kuongozwa na Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa
na Jakaya Kikwete kwa kutekeleza Ilani za Uchaguzi na Sera za CCM kama ilivyo sasa
kwa Serikali ya Awamu ya Tano.
Kuhusu madai kuwa eti Rais John Magufuli
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM hakiamini chama hicho nao ni upuuzi
unaopaswa kutupiliwa mbali na kupuuziwa huko.
CCM kama chama cha siasa, kwa mujibu wa
Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Toleo
la 2005 inayotumika sasa kina Katiba yake ambapo, yeye mwenyewe ni mmoja kati
ya maelfu ya wanachama wake waliopo nje na ndani ya nchi hii.
Aidha, Ibara ya 7 ya Katiba ya Chama Cha
Mapinduzi ya Mwaka 1977 Toleo la 2012 inayotumika hivi sasa nayo inasema: “Raia
yeyote wa Tanzania mwenye umri usiopungua miaka 18 anaweza kuwa mwanachama wa
Chama Cha Mapinduzi iwapo anakubali imani, malengo na madhumuni ya CCM” (mwisho
wa kunukuu).
Kama kifungu hicho cha Katiba ya CCM
kinaeleza hivyo na Rais Magufuli akiwa mwanachama wake hivi hata kwa akili
ndogo ya kisiasa ya Msigwa, ufahamu mfupi na hata vinginevyo inawezekanaje awe
hakiamini chama chake wakati “anakubali imani, malengo na madhumuni” yake?
Sikubaliani pia na madai ya kipuuzi ya
kiongozi huyo wa Chadema anapodai kuwa Rais John Magufuli “anafanya vitu
vinavyoofautiana na Chama Cha Mapinduzi”. Mbona hakuvitaja ili pia watu wengine
nao wavielewe na kupima ukweli wake, uzushi, uongo ama upotoshaji unaotaka
kupandikizwa ili kukidhi matakwa yake ya kisiasa?
Katika kuthibitisha uongo wa Msigwa,
Ibara ya 4 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inasema ifuatavyo:
“Katika miaka mitano ijayo (kwa maana ya
kuanzia mwaka 2015 – 2020), CCM ikiwa madarakani itaielekeza serikali yake
kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne (ambazo):
“Kwanza ni kuondoa umasikini, pili
kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira na hasa kwa vijana, tatu kuendeleza vita
dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma na nne, kuendelea kudumisha
amani, ulinzi na usalama wa maisha ya wananchi na mali zao”.
Aidha, Ibara ya 12 ya Ilani hiyohiyo
inasema lengo la mapambano dhidi ya rushwa ni “kuziba mianya ya rushwa katika
taasisi za umma, kuchukua hatua kali na za haraka kwa wote watakaobainika
kuendeleza rushwa serikalini na katika sekta binafsi, kuimarisha vyombo na
taasisi zinazohusika na kuzuia na kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja na
kuanzisha Mahakama Maalum kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi”.
Nayo Ibara ya 13 ya Ilani hiyo inasema “sambamba
na kupambana na tatizo la rushwa, serikali pia itatakiwa kushughulikia kwa ukali
zaidi tatizo la ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, matumizi mabaya ya
madaraka, ukiukwaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa umma, kuchelewesha
kutoa maamuzi yenye maslahi kwa umma na kusimamia uwajibikaji katika kutekeleza
masuala yenye maslahi kwa umma”.
Kutokana na hali hiyo na kulinganisha na
yale yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano akiwemo Rais John Magufuli
binafsi, hivi unawezaje kuja na udanganyifu kwamba haiamini CCM na kuwa eti
anafanya vitu vinavyotofautiana na chama hicho?
Baada ya haya yote ninaomba sasa nibainishe
ukweli kuwa Rais John Magufuli hajawatia hofu watu katika utekelezaji wa kazi
zake, utendaji wa serikali yake na hata vinginevyo, bali alichofanya ni kuvuruga
mianya ya wapinzani iliyotumika kufanyia uzushi na uongo kwa muda mrefu.
Safi sana!
Mwandishi
wa makala hii ni Katibu Msaidizi, Idara ya Itikadi na Uenezi katika Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam
What's up i am kavin, its my first time to commenting anyplace,
ReplyDeletewhen i read thjs piece of wroting i thought i could alo create comment duee
too this brilliant post.
This site was... how do you say it? Relevant!! Finally I've found something which helped me.
ReplyDeleteKudos!