Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai
wilayani Simanjiro wakati aliposimama akitoka Orkesimet kwenda
Mererani jana feb 16, 2017.
Mwananchi
wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro akiwasilisha kero yake kwa
njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho
waliokusanyika barabarani. Alikuwa akitoka Orkesimet kwenda Mererani jana
Februari 16, 2017.
Wananchi
wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka Orkesimet
kwenda Mererani
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mererani mkoani Manyara
wakati alipowasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara aliouhutubia
kwenye uwanja wa mikutano.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa
mikutano wa Mererani mkoani Manyara.
Baadhi
ya wananchi Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja
wa mikutano wa Mererani.
aziri
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango katika mikutano ya
hadhara ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa watendaji wa
Halmashauri hawawatembelei wananchi na kutatua kero zao.
Akihutubia
mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani mkoani
Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango
yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa
kumalizwa na viongozi hao na aliwaagiza kurejea Mererani siku
inayofuata ili waitishe mkutano na kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia
mkutano wa hadhara kwenye uwanja mikutano wa Mererani mkoani Manyara. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇