Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo mkoani Songwe
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi baada ya kutembelea mpaka wa
Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa
wahamiaji haramu wanaoingia nchini
kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.(Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇