LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 3, 2017

SHIRIKA: NDOA ZA UTOTONI BADO ZIPO IRINGA


 hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo.

hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP)



Na Fredy mgunda,Iringa
Shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.

    Akizungumza mjini Iringa,Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la wamasai bado ni kubwa.

Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya wamasai

     “Tunajitahidi kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu hasa huku umasaini”alisema Msigwa

      Aidha Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini  na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.

     “Sisi hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa

       Naye mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.

      “Mimi na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce

      Joyce ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.

      “Angalia tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema Joyce

      Zipo sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.

      Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula.

      Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA) umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages