Mlezi wa
Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
Taifa, Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini A, Unguja wakati wa
Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo.
Wana CCM
wa Kaskazini A wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya Uongozi
yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Kaskazini A Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya
kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi
yaliofanyika Mkokotoni Unguja kwenye Chuo cha Amali.
Na Mwandishi Maalum, Zanzibar
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na
watendaji wa CCM na Jumuiya zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi,
wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa Kaskazini (A) Unguja.
Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu chama kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia CCM kusonga mbele na kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.
Amesisitiza
wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na
mikakati imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na
kushika dola.
Mjumbe
huyo ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini A Unguja
amesema Umoja na Mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio
silaha madhubuti itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na
kuongeza maradufu idadi ya wanachama nchini.
Amesema
kwa sasa Viongozi watakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha
jumuiya za chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri
ili zianze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za
chama.
Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa pia ameendelea kuonya
baadhi ya viongozi waache tabia ya kutengeneza makundi ya ndani ya chama
kwa ajili ya kusaka madaraka bali wawe mstari wa mbele katika kujenga
umoja na mshikamano ndani ya chama.
Kuhusu
mafunzo, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wanaopata mafunzo hayo
kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi kwenye maeneo yao wanafanya
kazi kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa.
Amesema
kwa sababu Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya Chama cha
Mapinduzi ni muhimu kwa viongozi wa chama katika ngazi zote washirikiane
na viongozi wa Serikali katika maeneo husika ili kuhakikisha miradi ya
maendeleo ya wananchi inafanyika kwa ubora unaotakiwa kulingana na
thamani ya fedha.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇