Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amekutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Martin Bille
Herman, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na
Balozi wa Denmark hapa nchini Mhe. Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Mpango.
Martin Bille Herman amesema
katika mazungumzo hayo wamejadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo
kati ya Tanzania na Denmark na pia wamekubaliana kuuimarisha zaidi hususani
katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.
Wakati
huo huo, Rais
Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mkapa amesema lengo la
kukutana na Mhe. Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji
wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇