Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Rais Dk. John Magufuli, leo amemtumbua Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzia leo, Januari Mosi, 2017.
Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amefanya 'bandika bandua' kwa kumteua Dk. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO.
"Kabla ya uteuzi huo Dk. Tito Esau Mwinuka alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na
uteuzi wa Dk. Tito Essau Mwinuka unaanza mara moja", imesema taarifa hiyo ya Ikulu iliyosainiwa ana Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa.
Hatua ya Rais Magufuli, imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.
Ongezeko hilo lilitangazwa juzi jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maombi ya kurekebisha bei za umeme ambayo yalitarajiwa kuanza... inaendelea/>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇