Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi
zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF)
zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya
Mapinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akihutubia mara tu alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa
ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya
maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
ndani ya moja ya nyumba hizo 252 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa nyumba hizo za Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar
(ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53
ya Mapinduzi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiangalia ramani ya ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na
Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni,
Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Pichani
ni Nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar (ZSSF) zitakazokuwa na nyumba 252, Viwanja vya Michezo kwa
Watoto,Sehemu ya kuogelea na Ukumbi mkubwa.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimia wananchi waliojitokeza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
la ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya
maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Sehemu ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Hassan Suluhu
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akfurahia jambo na wanafunzi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la
msingi la ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar
ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan
ameuagiza uongozi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uchangamkie
fursa za uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Bara hasa
kwenye Makao Makuu ya nchi Dodoma hatua ambayo itauwezesha mfuko huo
kuongeza maradufu mtaji wake kwa uuzaji wa nyumba hizo.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anaweka jiwe la
msingi katika mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi katika eneo
la MBWENI kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa
Rais amesema kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo
wa ZSSF hasa ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi ni muhimu kwa mfuko
huo kuangalia namna bora ya kwenda kuwekeza katika mikoa mbalimbali ya
Tanzania bara kutokana maeneo mengi kuwa na mahitaji makubwa ya nyumba
za makazi.
Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania
Zanzibar ulitokana na fikra na ahadi za hayati mzee Karume kupitia ASP
wakati wa haraka za kudai uhuru za kuhakikisha wananchi wanapata makazi
bora ya kuishi katika kisiwa cha Pemba na Unguja kutokana na idadi kubwa
ya wananchi katika kipindi hicho kuishi katika mazingira
yasiyoridhisha.
“Miradi
yote hii ni katika kuenzi utekelezaji wa kauli ya Mapinduzi Daima
yanayotaka kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi kila uchao
hususani kipindi hiki tunapotimiza miaka 53 ya Mapinduzi yetu ya
Matukufu ya Zanzibar”
Makamu wa
Rais pia amewahimiza wananchi wote wachangamkie fursa za kununua na
kumiliki nyumba kwa bei nafuu na zenye miundombinu ya kisasa na huduma
zote za kijamii ikiwemo viwanja vya michezo.
Kuhusu
umiliki wa nyumba kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara
zinazoshughulika na masuala ya ardhi Tanzania Bara na Zanzibar kutoa
ufafanuzi au tafsiri sahihi ya sheria zinazoongoza masuala ya ardhi na
umiliki wa nyumba ili kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu wana diaspora
kumiliki nyumba.
Amesisitiza
kuwa Serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza wana diaspora kuchangia
maendeleo ya nchi na kutumia fursa mbalimbali zilizoko nyumbani ikiwemo
kununua nyumba zinazojengwa na mifuko na mashirika mbalimbali hivyo ni
muhimu kwa wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoa maelekezo
haraka ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwa sasa kuhusu wana diaspora
kulimiki nyumba kwa ajili ya makazi.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa mifuko
hiyo kuwekeza katika sekta ya viwanda hasa kwenye miradi yenye tija
kwani viwanda vitatoa fursa kwa vijana wengi kuajiriwa na kuongeza
kipato na kuongeza huduma za kijamii na kupunguza umaskini kwa wananchi.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipngo wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dkt Khalid Salum Mohamed amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa
Serikali hiyo inaendelea kumuezi Mzee Karume kwa vitendo kwa kujenga
nyumba za makazi na kukarabati nyumba zilizopo ili kuhakikisha wananchi
katika Kisiwa cha Pemba na Unguja wanapata makazi bora ya kuishi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇