“Historia ya Maisha yangu ni ndefu kama ilivyokwisha elezwa. Nilizaliwa Kijijini, nikasoma Kijijini na mjini na nikafanya kazi vijijini na mjini. Katika Maisha yangu yote nimetekeleza kwa nadharia na vitendo falsafa ya UMOJA Ni NGUVU.
Vitendo vimejidhihirisha zaidi katika vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika na katika vyama vya siasa, hususan Tanganyika African National Union (TANU) na Baadaye Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika Utendaji kazi, nilizingatia falsafa hii ya UMOJA NI NGUVU”.
Nikiwa na umri wa mika 23 na mtumishi Serikalini, nilijiunga na Chama cha Watumishi Waafrika Serikalini (Tanganyika African Government Servats’ Association-TAGSA). Nilijiunga na chama hicho cha wafanyakazi kwa imani kwamba UMOJA NI NGUVU. Sikuona njia nyingine ya kupambana na dhuluma za Mkoloni kwa wafanayakazi Waafrika ila kuungana na kuanzisha vyama vya wafanyakazi. Niliamini kwamba..... Inaendelea/>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇