Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu msaada wa dola za Kimarekani 50,000/= sawa na
shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya
Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo
umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi
yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9
septemba 2016.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kulia) akipokea
mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Kimarekani 50,000/= sawa na
shilingi milioni 108 za Kitanzania zilizotolewa na Balozi wa Jamhuri ya
Korea nchini Bw. Song, Geum-young leo jijini Dar es Salaam. Msaada huo
umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na makazi
yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9
septemba 2016.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Balozi Dkt. Agustine Mahiga (kushoto) akiagana
na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum-young mara baada ya
kupokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 leo jijini Dar es Salaam.
Msaada huo umetalewa kwa ajili ya kusaidia kurejesha miundombinu na
makazi yaliyoathiriwa na Tetemeko la ardhi Mkoani Kagera mnamo tarehe 9
septemba 2016. Picha na MAELEZO.
Na: Frank Shija – MAELEZO.
Tanzania
yadhamiria kuimarisha uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa
kufungua Ofisi zake za Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.
Hayo
yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati
akipokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 kwa ajili ya kusaidia
urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika kutokana na Tetemeko la Ardhi
lilitokea Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 Septemba 2016.
Balozi
Mahiga amesema kuwa nchi ya Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri
na wa muda mrefu na Tanzania ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa
ikisaidia katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
miundombinu ya afya akitolea mfano Hospitali za Mloganzila na Chanika
ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Mahusiano
la Korea (KOICA).
“Korea
imekuwa na Ofisi za Ubalozi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo
wameona ni wakati sasa kwa Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini
nnchini Korea,” Alisema Balozi Mahiga.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young
amesema kuwa msaada huo unatokana na namna ambavyo waliguswa na janga la
Tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu
mkubwa wa miundombinu na makazi ya wananchi.
Ameongeza
kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais
Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22
Septemba mwaka huu.
Balozi
Song Geum-Young pia amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza
na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa
kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini
ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila,
Chanika na mingineyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇