Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli amehitimisha sherehe za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika, katika shamrashamra zilizofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Akihutubia katika sherehe hizo, Dk. Magufuli amesema mambo kadhaa, akitangulia kusema, kwamba sherehe za mwaka huu, huenda ndiyo zikawa za mwisho kufanyika jijini Dar es Salaam.
Dk. Magufuli amesema, badala ya kufanyika Dar es Salaam, mwakani sherehe hizo zitafanyika Dodoma ambayo ndiyo Makao Makuu ya Nchi.
Amewataka wakazi wa Dar es Salaam, wanaopenda burudani ya gwaride la Majeshi ya Ulinzi na Usalama, mwakani kusafiri kwenda Dodoma ili kuona burudani hiyo.
"Nadhani wale wakazi wa Dar es Salaam, wanaopenda burudani hii ya gwaride la majeshi yetu, mwakani watalazimika kusafiri kwenda Dodoma ili kuiona burudani hii nzuri", alisema, Rais Dk. Magufuli.
Rais Magufuli alieleza kuwa sherehe alizohudhuria leo ni za mara ya pili ingawa mwaka jana hazikufanyika kama leo.
"Najua wapo watakauliza, nasemaje hii nimehurudhuria shere ya pili wakati mwaka jana haikufanyika, lakini ukweli sherehe ilifanyika ispokuwa tuliifanya kwa kufanya shughuli za usafi",
"Niliamua hivyo kwa sababu nipouliza gharama niliambiwa ni sh. bilioni nne, nikauliza fedha hizi nikwa matumizi gani, nikaambiwa ni kwa ajili ya wageni, posho na chakula. Nikauliza je chakula hiki kitaliwa na Watanzania wote? Nikaambiwa hapana. Basi nikaamua fedha hizo zitumike kutengeneza barabara ile ya Ali Hassan Mwinyi inayoenda kule Mwenge ambayo itatumiwa na Watanzania wengi." Alisema, Rais Dk. John Magufuli na kuongeza;
"Najua wapo waliokwazika na uamuzi lakini kama wapo naomba mnisamehe, na leo baada ya sherehe hizi hapa Uwanjani tumemalizana hakuna shughuli nyingine" Alisema Rais Dk Magufuli.
Sherehe hizo ambazo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mama samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phili Mangula na Mwenyekiti wa CUD Profesa Ibrahim Lipumba, zilishereheshwa kwa gwarige, ngoma za burudani na kwaya. >>ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI PICHA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, leo Desemba 9, 2016 amewaongoza
mamilioni ya watanzania kusherehekea Uhuru wa Tanzania Bara kwenye
uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo kivutio kikubwa kilikuwa
kikosi maalum cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, Makomandoo
ambapo pamoja na kuonyesha umahiri wao katika medani za kivita, lakini
kubwa ni komandoo hao kulala juu ya misumari yenya ncha huku wengine
wakimkanyaga mwenzao aliyelalia misumari, kifuani. Pichani Komandoo huyo
akionyesha maajabu hayo. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Komandoo wakionyesha jinsi ya kupambana na adui bila ya kutumia silaha
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Dk. John Magufuli, akikagua gwaride la vikosi vya majeshi hayo wakati wa maadhimisho hayo.
Paride la kimyamimya |
Amiri Jeshi waMjeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru akiwa kwenye gari la wazi la Kijeshi
Amiri Jeshi waMjeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais John Magufuli, akiwa na Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange, akiwapungia wananchi wakati akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru akiwa kwenye gari la wazi la Kijeshi |
Wakati Rais Dk Magufuli akitoa hotuba yake
Rais Dk Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa katikati ni Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein |
Rais Dk Magufuli akionyesha furaha wakati akikagua gwaride kikosi cha Brass Band |
Rais wa zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akimsalimia Jaji Mkuu. Katikati ni Waziri Mkuu |
Baadhi ya wananchi wakitazama kutokea uwanja waTaifa kilichokuwa kikiendelea kwenye uwanja wa Uhuru
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
Rais akipigiwa mizinga na wimbo wa Taifa |
Rais akiagana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda |
Rais akisindikizwa na Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani waliokuwa wakitembea naye kwa miguu wakati akiondoka Uwanjani |
Rais Dk Magufuli akisalimiana na Mzee Mwinyi |
Rais akiwaaga wananchi baada ya sherehe |
Rais Dk. John Magufuli akiagana na Mjane wa Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kabla ya kuondoka Uwanjani/ Hotoba ya Rais Magufuli/BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇