LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 4, 2016

RAIS DK MAGUFULI NA MKEWE KUTOA SH. MILIONI TANO KUSAIDIA MTOTO ANAYEUGUA MBAGALA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Rais Dk. John Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, wameahidi kutoa mchango wa Sh. Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto mwenye umri wa miaka saba, Haidari Bonge  anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, mdomoni na machoni.

Mtoto huyo anayeishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam, alianza kuotwa nyama miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara. 

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam, imesema, Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo baada ya kutazama kipengele cha Hadubini “Habari kwa Kina” kilichokuwa kikionyeshwa na Kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji Tanzanaia (TBC), katika taarifa ya habari ya kituo hicho ya saa 2 usiku jana, Desemba 3, 2016.


“Mimi na Mke wangu tumeguswa na tatizo linalomkabili mtoto huyu, Hidari Bonge na tumeamua kuchangia Shi Milioni 5 kutoka kwenye mshahara kwa ajili ya kuchangia matibabu yake.

“Pia tunatoa pole kwake na kwa familia yake ambayo imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuhakikisha anapatiwa matibabu kwa kipindi kirefu cha miaka saba sasa” Taarifa hiyo imemkariri Rais Magufuli akisema na kuahidi kuukabidhi mchango huo leo, Desemba 4,, 2016.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages