Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili
mkoani humo. Pia Rais Dkt. Magufuli anatarajiwa kushiriki katika Ibada
ya Krismasi mkoani humo hapo Kesho.
.Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu
cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa
Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja
na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika
Kanisa mojawapo mkoani Singida. PICHA NA IKULU
TAARIFA
TAARIFA
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 24
Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa
huo Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Singida.
Rais
Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, kesho tarehe 25 Desemba 2016
wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini
katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani Singida.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba
waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi
kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni
heshima kwao kutokana na uwepo wa Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu
ya Krimass.
Dkt.
Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla
kuendelea kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee
kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Amesema
ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea
Kiongozi huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia
ulimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Kassim Majaliwa alipohudhuria sherehe za Maulidi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇