Na Is-haka Omar, Zanzibar.
MGOMBEA mteule wa Tiketi ya CCM jimbo la Dimani Unguja, Juma Ali Juma amewashukuru na kuwapongezi viongozi wa ngazi zote za chama hicho kwa jinsi walivyoendesha mchakato wa uteuzi wake.
Mteule huyo ambae alitangazwa kati kati wa wiki hii baada ya kikao cha Kamati Maalum ya halmashauri kuu ya CCM zanzibar alikuwa ni miongoni mwa makada 25 wa chama hicho waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza na Gazeti hili jana mgombea huyo alisema anavipongeza vikao hivyo vya CCM kwa kumuamini kumpa jukumu la kupeperusha bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi mdogo wa jimbo hilo na kuahidi kutekeleza wajibu huo kikamilifu.
Alieleza kuwa katika kutimiza wajibu huo kwa chama chake na wanancnhi kwa ujumla, atahakikisha analinda, anaheshimu na kukiwakilisha vyema Chama chake katika uchaguzi huo.
“Chama Cha Mapinduzi kupitia watendaji, viongozi, makada na wachama wake wote walioshirikiana kwa njia moja ama nyingine kuanzia hatua za awali mpaka nateuliwa nawashukru sana kwa hekima na busara zao hakika sitowaangusha popote nitakaposimama kunadi sera za chama na serikali iliyopo madarakani.
Akizungumzia ushindani katika mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama, Juma alisema ulikuwa mkubwa uliotawaliwa na demokrasia, uhuru na maamuzi yaliyojaa busara.
“Ushindani uliokuwepo katika uchaguzi wa ndani ya chama ni kipimo tosha cha kunifanya niamini kuwa walioniteuwa wamejiridhisha kuwa nafaa kuvaa viatua vya alikuwa Mbunge wa jimbo hili marehemu Tahir (Hafidh Ali).”, alieleza Juma.
Sambamba na hayo mteule huyo aliweka wazi baadhi ya mambo atakayoyapigania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anasimamia utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa manufaa ya wananchi wa jimbo hilo bila ya ubaguzi.
Jumla ya vyama viwili Zanzibar vimetangaza nia ya kushiriki katika uchaguzi huo ambavyo ni Chama Cha Wananchi (CUF) na CCM ambavyo vimekamilisha mchakato wa kumpata mgombea katika uchaguzi huo unaofanyika baada ya kifo cha aliekuwa Mbunge wa jimbo hilo marehemu Hafidh Ali Tahiri aliyefariki mwezi uliopita mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇