Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 |
Gereza
kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia jana jioni moshi ulikuwa bado unaendelea kutanda huku kilichosababisha moto huo kikiwa bdo hakikajulikana.
Shughuli
za kuzima moto zilikuwa bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi
vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.
Hilo ni
gereza linalohifadhi wafungwa mchanganyiko wakiwemo wale wa kisiasa na wengine
wa mauaji ya kimbari.
Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka minne iliyopita kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka minne iliyopita kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.
Viongozi kadhaa serikalini wakiwemo mawaziri na wakuu wa majeshi na ulinzi na polisi wamefika kwenye eneo la tukio
Bado ni
mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari
hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza hilo kuu ya Kigali.
Magari ya
zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa
wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa. BBC
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇